Home Simba SC KAIZER CHIEFS WAMTAKA GOMES KUVAA VIATU VYA HUNT

KAIZER CHIEFS WAMTAKA GOMES KUVAA VIATU VYA HUNT


Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes da Rosa yupo kwenye rada za kuchukuliwa na timu kigogo kutoka Afrika Kusini , timu ya Kaizer Chiefs.

Kaizer Chiefs ambao wamemfuta kazi kocha wao mkuu,Guvin Hunt hivi karibuni, inasemekana wako kwenye mpango wa kumchukua Gomes kwenda kuziba nafasi ya kocha huyo aliyewaingoza kufinga hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Afrika.

Kaizer Chiefs walimfuta kazi Hunt kutokana na kushindwa kuifanya timu hiyo kongwe Afrika Kuisni kufanya vyema kwenye ligi kuu nchini humo pamoja na mashindano mbalimbali ya ndani.

Taarifa kutoka Afrika Kusini ,zinasema kuwa Kaizer Chief wanamtazama Gomes kama mrithi sahihi wa Hunt kutokana na namna ambavyo ameifanya Simba SC kuwa timu tishio barani Afrika kwa kuzifunga timu kubwa na kucheza soka safi .

Aidha, mabosi wa Kaizer wanaona Gomes ataifanya timu hiyo kuwa tishio kwenye ligi kuu na michuano ya kimataifa pamoja na kuifikisha timu hiyo Final ya Klabu Bingwa Afrika Msimu huu.

Chanzo kutoka nchini humo, kinasema kuwa Kazier wameshaanza kuwasiliana na wakala wa kocha huyo kutoka Ufaransa kwa ajili ya kujiunga nao kabla ya mechi za nusu fainal ya Klabu Bingwa Afrika.

Hata hivyo inawezekana Kazier wakapa ugumu kumng’oa Gomes kwenye timu yake ya sasa kutokana na imani kubwa ambayo imeonyeshwa kwake na mabosi wa klabu hiyo ambayo kwa muda mfupi amefanya mambo makubwa ikiwemo kuiwezesha Simba SC kuingia hatua ya Makundi na robo fainal ya Klabu Bingwa Afrika.

Pia, ugumu watakaopata Kaizer Chiefs ni pamoja na kuuvunja mkataba wa kocha huyo na klabu yake ya sasa, itakumbukwa kuwa Gomes alisaini mkataba wa miaka miwili na Simba SC mwezi wa pili mwaka huu.

Hata hivyo, hivi karibuni akiwa Afrika Kusini na Simba SC kwenye mechi ya Robo Fainal ya Klabu Bingwa Afrika, Gomes aliulizwa swali na waandishi habari kuhusu uwezekano wa yeye siku moja kufundisha timu za huko, ambapo alijibu kuwa kila jambo linawezekana ila kwa sasa yupo na Simba SC na anafurahia maisha ndani ya klabu hiyo kwa sasa.

SOMA NA HII  PATRICK AUSSEMS AIPA NAFASI SIMBA KUTINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Gomes alisema kuwa, kwa sasa bado ana mipango mingi ya kufanya ndani ya timu yake ya sasa, hivyo kama kuondoka itambidi kumaliza kwanza mipango hiyo.

Pamoja na hayo, Didie Gomes Da Rosa hana historia ya kudumu na timu muda mrefu haswa pale anapopata dili jipya na zuri, itakumbukwa kuwa alikuwa kocha wa AC Cannes B ya Ufaransa, ambapo hakumaliza mkataba wake kabla ya kujiunga na Timu nyingine nyingi kwa muda mfupi mfupi ,mpaka Simba SC walipomchukua kutoka klabu ya El Merikh ya Sudani.