Home Simba SC MWENYEKITI MPYA SIMBA ASHINDA KWA ASILIMIA 70

MWENYEKITI MPYA SIMBA ASHINDA KWA ASILIMIA 70

 LEO Februari 7, Simba imepata Mwenyekiti mpya ambaye anakuwa mrithi wa mikoba ya Sued Mkwabi ambaye alibwaga manyanga Septemba 2019.

Uchaguzi wa leo ambao umefanywa na Wanachama waliokidhi vigezo ikiwa ni pamoja na kulipa ada ya uanachama umefanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere.

Mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba ni Murtaza Mangungu baada ya kupata kura 802 (70.35%) akimshinda Juma Nkamia aliyepata kura 330 (28.95%).

Jumla ya kura zilizopigwa ni 1140 na kura 8 (0.7%) zimeharibika.

SOMA NA HII  KISA AKPAN KUSAJILIWA SIMBA...KOCHA WAKE WA ZAMANI AIBUKA NA MADAI HAYA...