Home Yanga SC YANGA: TUNAWAHESHIMU WAPINZANI WETU ILA TUTAPAMBANA NDANI YA UWANJA

YANGA: TUNAWAHESHIMU WAPINZANI WETU ILA TUTAPAMBANA NDANI YA UWANJA


 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City unaotarajiwa kuchezwa Februari 13, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Yanga ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa wamecheza jumla ya mechi 18 bila kupoteza na kibindoni wamekusanya jumla ya pointi 44. wameshinda mechi 13 na sare tano.

Kaze amesema kuwa kila mchezo kwao ni fainali na wanatambua kwamba wapinzani wao wamejipanga kupata ushindi jambo ambalo halimpi tabu.

“Kila mchezaji anajua majukumu yake akiwa ndani ya uwanja, nina waamini vijana wangu wanafanya kazi vizuri wakiwa ndani ya uwanja hivyo ni muhimu kwetu kushinda.

“Jambo zuri ni kwamba hakuna ambaye anajua nini kitatokea kesho sisi tunaangalia maandalizi yetu pamoja na nguvu kubwa kwenye kusaka ushindi ndani ya dakika 90.

“Tunawaheshimu Mbeya City ni timu nzuri ipo wazi ila haitatufanya tuingie uwanjani kwa kujiamini, kila kitu kitakuwa sawa ndani ya uwanja mashabiki watupe sapoti,” amesema.

SOMA NA HII  KISA LIGI KUU..YANGA WAVUNJA MAKUBALIANO NA MCHEZAJI HUYU WA KIMATAIFA..UONGOZI WATO TAMKO...