Home Uncategorized GSM KUMWAGA MKWANJA WA MAANA KWA WACHEZAJI WASEPE NA KOMBE LA SHIRIKISHO

GSM KUMWAGA MKWANJA WA MAANA KWA WACHEZAJI WASEPE NA KOMBE LA SHIRIKISHO

INJINIA, Hersi Said, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, amesema kuwa watatoa mkwanja wa maana kwa wachezaji ili kuwaongezea morali ya kupambana kubeba taji la Kombe la Shirikisho.

Yanga ipo hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo kati ya Julai 27/28 itamenyana na Kagera Sugar endapo itashinda itakutana na mshindi kati ya Simba ama Azam FC.

Said amesema:-Tutatoa mkwanja mrefu kwa ajili ya kuwapa morali wachezaji ili wapambane kwa ajili ya kuhakikisha tunabeba taji la Kombe la FA.

 “Malengo yetu ni kuona kwamba timu inarejea kimataifa na inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika hivyo suala la bonasi hilo lipo kwa wachezaji kuhakikisha ushindi unapatikana,” amesema.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA GWAMBINA FC KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA SIMBA UWANJA WA MKAPA