Home Uncategorized KIUNGO YANGA AWAHAKIKISHIA WANACHAMA KUICHAKAZA ZESCO

KIUNGO YANGA AWAHAKIKISHIA WANACHAMA KUICHAKAZA ZESCO


Nahodha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Papy Tshishimbi amesema wanajiandaa vema kuhakikisha wanashinda mchezo wa nyumbani kabla ya kurudiana nchini Zambia kwa wapinzani wao, Zesco United.

Yanga inatarajiwa kuvaana na Zesco katika mchezo wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kati ya Septemba 13 hadi 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo imefanikiwa kufuzu kucheza hatua hiyo baada ya kuwaondoa Township Rollers ya Botswana nyumbani kwao kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Mganda, Juma Balinya.

Tshishimbi alisema kuwa hesabu zao ni kufi ka hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa Afrika.

Tshishimbi alisema kuwa hawataki kurudia makossa waliyoyafanya kwenye mchezo dhidi ya Rollers ya kuruhusu bao nyumbani na zaidi wamepanga kupata ushindi pekee katika mechi zote mbili.

Ameongeza kuwa kitendo cha wao kuruhusu bao nyumbani kiliwafanya wacheze kwa presha kubwa ugenini, licha ya ushindi wa bao 1-0 walioupata huko Botswana.

“Kikubwa tulichopanga kuwa ni kufunga na sisi tusifungwe kama ikishindikana hilo, basi tupate suluhu nyumbani na hilo linawezekana kutokana na maandalizi tunayoendelea kuyafanya.

“Tunaanzia nyumbani,hatupaswi kufanya makossa kama ilivyokuwa mchezo dhidi ya Rollers, tunahitaji ushindi na nzuri Zaidi kupata bao la mapema litakalowapa presha wapinzani wetu.

“Ushindi wa nyumbani utatupungizia presha ya mchezo wa ugenini, hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kufuzu makundi, tumejiwekea malengo ya kuingia hatua ya makundi na lolote linaweza kutokea tukishaingia hatua hiyo,” alisema Tshishimbi.

SOMA NA HII  SERIKALI YAZUNGUMZIA SIMBA NA YANGA,KESHO NDANI YA CHAMPIONI JUMATANO