Home Uncategorized TSHISHIMBI KUFIKISHA YANGA HATUA WALIYOFIKA SIMBA CAF

TSHISHIMBI KUFIKISHA YANGA HATUA WALIYOFIKA SIMBA CAF


Papy Tshishimbi ambaye ni nahodha wa timu ya Yanga  kwa sasa ameweka msisitizo wa timu yake kufika katika rekodi ambayo iliwekwa na wapinzani wao wa jadi, Simba, msimu uliopita kwa kucheza hatua ya makundi.

“Tunataka kufika katika makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hilo ndiyo lengo letu ambalo tumejiweka wachezaji kwa sasa.

“Tunajua itakuwa mechi ngumu tutakapopambana  na Zesco lakini tutapambana kuona tunashinda na kutinga kwenye makundi kama kila moja anavyotamani hapa,” alisema Tshishimbi.

Yanga inakutana na Zesco baada ya kuitupa nje Township Rollers katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 2-1.

SOMA NA HII  OKTOBA 25, LIGI KUU BARA RATIBA IPO HIVI LEO