Home Habari za michezo WAKATI TETESI ZA KUFUKUZWA ZIKIWA BADO ZA MOTO..NABI HUYU HAPA AFUNGUKA KUHUSU...

WAKATI TETESI ZA KUFUKUZWA ZIKIWA BADO ZA MOTO..NABI HUYU HAPA AFUNGUKA KUHUSU SIMBA…

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kitendo cha watani wao wa jadi, Simba kushindwa kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa juzi Jumapili ni wazi kuwa hawawezi kumpata tena, amefunguka hayo na kukiri kuwa wapinzani wake walikuwa bora.

Yanga ilikuwa mwenyeji wa mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam ukimalizika kwa sare ya bao 1-1 mabao yote yakifungwa kipindi cha kwanza na Augustine Okrah na Stephane Aziz KI.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika Nabi alisema; “Nilitegemea watatufunga kutokana na ubora wao waliouonyesha hasa kipindi cha kwanza lakini mara baada ya kukaa na wachezaji mambo yalibadilika na sisi tulitengeneza nafasi kipindi cha pili wachezaji walishindwa kuzitumia.

“Kila timu ilistahili pointi moja tuliyogawana kutokana na vipindi, wao walikuwa bora zaidi kipindi cha kwanza na sisi tulikuwa vizuri kipindi cha pili kama kila upande ungeongeza umakini ni mabao mengi zaidi yangepatikana kwasababu kila mmoja alitengeneza nafasi.”

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda alisema wachezaji wake walicheza vizuri ni presha ndio iliyosababisha washindwe kupata matokeo kwenye mchezo huo huku akisisitiza ataendelea kuyfanyia kazi mapungufu waliyoyaonyesha ili waweze kuwa bora zaidi.

“Kila inapotokea mechi ya Simba na Yanga mambo mengi yanatokea pamoja na ukongwe wa mechi hii bado wachezaji wanakuwa na presha, wachezaji wangu kama wangetuliza akili zao tulikuwa tunaibuka na ushindi walitengeneza nafasi nyingi walishindwa kuzitumia,” alisema na kuongeza;

“Tumesahau matokeo haya sasa tunaangalia mechi inayofuata dhidi ya Azam FC malengo ni kuendelea kukusanya pointi ili tuweze kujitengenezea mazingira mazuri ya kutwaa taji la Ligi Kuu msimu huu.” Mchezo wa Azam na Simba utafanyika Uwanja wa Mkapa Alhamisi saa 1:00 usiku.

SOMA NA HII  SARR AIBUA VITA MPYA SIMBA....MABOSI WAKUNA KICHWA...CHAMA, KRAMO NA PHIRI KUCHUNJWA...