Home Habari za michezo ZAHERA: ‘MIMI SIO SHABIKI WA YANGA’…AFUNGUKA A-Z KUHUSU ISHU YA MKATABA WAKE…

ZAHERA: ‘MIMI SIO SHABIKI WA YANGA’…AFUNGUKA A-Z KUHUSU ISHU YA MKATABA WAKE…

Kocha wa Soka, Mwinyi Zahera raia wa Congo DR amefunguka kuwa amemaliza mkataba wake ndani ya Klabu ya Young Africans SC.

kauli hiyo ya Zahera inakuja baada ya kuonekana katika vyombo vya habari akiwasema baadhi ya wacheaji wa Yanga kama beki Djuma Shaban kuwa unene unamuangusha.

“Mimi ni Yanga naipenda sana Yanga, mkataba wangu na Yanga umemalizika, uliisha Septemba 30, 2022.

“Japo mkataba umeisha lakini bado naweza kwenda Yanga hata kushauriana na viongozi hakuna tatizo lolote hata kocha Nabi naongea nae vizuri tu.

“Mimi ni Yanga sio shabiki, siisemi Yanga vibaya mimi naishauri kiufundi kama kocha. Naipenda Yanga ndio maana natoa ushauri,” amesema Mwinyi Zahera.

SOMA NA HII  HISTORIA YA 50 CENT NA UTAJIRI ANAOMILIKI...SHINDA MAMILIONI KUPITIA MERIDIANBET...