Home Habari za michezo AHMED ALLY : YANGA WATATOLEWA TU…WANATAKIWA KUWA NA CHAMA ILI WASHINDE KESHO…

AHMED ALLY : YANGA WATATOLEWA TU…WANATAKIWA KUWA NA CHAMA ILI WASHINDE KESHO…

Habari za Michezo leo

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Klabu ya Simba SC Ahmed Ally ameitakia kila la kheri Young Africans kuelekea mchezo wa Hatua ya Mtoano Kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain ya Tunisia.

Young Africans itakua mwenyeji wa Mchezo wa Mkondo wa Kwanza utakaorindima Uwanja wa Benjamin Mkapa kesho Jumatano (Novemba 02), huku ikihitaji ushindi utakaoiweka kwenye mazingira mazuri ya kuelekea mchezo wa Mkondo wa Pili utakaopigwa Novemba 09 mjini Tunis-Tunisia.

Ahmed Ally ametuma salamu hizo za kheri, huku akiipiga kijembe Young Africans kwa kusisitiza salamu hizo zitawafaa kama wamejiandaa kushinda na sio kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho.

“Tunawatakia kila la kheri, lakini kama wamejiandaa. Kama hawajajiandaa watatolewa tu.”

“Siri ya kufanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa ni kuwa na kina Chama, Phiri, Mkude, Sakho. Young Africans hawana watu kama hao ndiyo maana hawafanyi vizuri Kimataifa” amesema Ahmed Ally

Jana Jumatatu (Oktoba 31) Ahmed Ally alirusha kijembe kwa watani zao wa jadi kupitia Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii akiandika: Mara ya mwisho Mtani kushiriki makundi ya ligi ya mabingwa Afrika, Watanzania tulikua Milioni 30, sasa hivi tupo milioni 61 kwa iyo watanzania Milioni 31 hatujawaona wakicheza makundi yaani nusu ya nchi hatujawahi kuiona UTOPWA makundi

Tayari Simba SC imeshatinga hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, baada ya kuifunga na kuitoa Primeiro de Agosto ya Angola kwa ushindi wa jumla wa 4-1.

Young Africans itatakiwa kushinda mchezo dhidi ya Club Africain, ili itimize lengo la kucheza hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu 2022/23.

SOMA NA HII  MASAU BWIRE - FURAHA KWA WATANZANIA NI SIMBA KUPATA USHINDI WA KISHINDO LEO...