Habari za Simba
Habari za michezo

BAADA YA KUONA MWAMNYETO ‘ANAZINGUA’ KILA AKIPANGWA…KAZE AAMUA KUJIMALIZA KWA BACCA…

admin November 2, 2022 6:13 am

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema Ibrahim Bacca amewaongezea wigo katika machaguo ya wachezaji wa kuwatumia kwenye safu ya ulinzi.

Bacca ameonyesha utayari wa kutumika katika kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa shirikisho dhidi ya Club Africain baada ya kuwa na kiwango kizuri katika mechi mbili zilizopita dhidi ya KMC na Geita Gold

“Bacca amecheza vizuri mechi zilizopita hili jambo jema kwake na timu kwa ujumla kwani ametuongezea ubora kwenye safu ya ulinzi”, alisema

Baada ya nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto kukabiliwa na matatizo ya kifamilia, Bacca anaonekana kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuanza mbele yake baada ya kuonyesha ubora katika mechi alizopewa nafasi

Dickson Job na Bacca wameonyesha ‘ukatili dhidi ya washambuliaji wa timu pinzani licha ya maumbile ya miili yao kuwa madogo.

ILI KUEPUKA MAKOSA TENA…NABI KAONA ISIWE TABU…KAPANGA KUTUMIA MBINU HIZI ZA SIMBA LEO… WASHINDI WA PROMOSHENI YA BODABODA NA SIMU WAPATIKANA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply