Habari za michezo

NABI: HUU NI MPIRA..AZIZI KI NI ZAIDI YA FEI TOTO UWANJANI…

admin November 3, 2022 6:48 pm

Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi amesema Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burkina Faso Stephen Aziz Ki, anazidi kuimarika kutokana na uwezo ambao ameuonesha kwenye Michezo iliyowakabili msimu huu 2022/23.

Ndani ya Ligi Kuu Tanzana Bara, Kiungo huyo ameshacheza michezo saba kati ya nane, akitumia dakika 468, ametupia mabao mawili, ana pasi moja ya bao.

Kocha Nabi amesema kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji wanaofanya vizuri katika kikosi chake na ametoa mchango mkubwa katika ushindi walioupata kwenye michezo ya Ligi Kuu.

“Aziz Ki ni miongoni mwa wachezaji wazuri ambao wanafanya kazi kubwa kwa ushirikiano, nasikia mashabiki wanalalamika kuhusu nafasi anayocheza, muda mwingine wanasema ninamchezesha nafasi ya Feisal Salum, hapana, huu ni mpira.”

“Kila mchezo unahitaji mbinu yake ya ushindi, hivyo wanapopewa majukumu wanatimiza kwa kushirikiana, kabla ya mchezo huwa ninaangalia wapinzani wanafanyaje na nina wachezaji wa aina gani, hapo tunakwenda kuwakabili,” amesema Nabi.

Aziz Ki alisajiliwa Young Africans mwanzoni mwa msimu huu, akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Mabingwa wa Soka Ivory Coast ASEC Mimosas.

BAADA YA YANGA KUCHEZA VIBAYA JANA…SHAFIIH DAUDA KATOA USHAURI HUU KWA FEI TOTO… MGUNDA AJIPA UJIKO KUHUSU OKRAH…” MIMI NDIYE NIMEBADILISHA..HAKUWA HIVI HUKO NYUMA”…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply