Habari za Yanga
Habari za Yanga

KISA MASHABIKI KULALAMIKA SANA KUHUSU UWEZO WA NABI…YANGA WAFANYA MAAMUZI HAYA MAGUMU…

admin November 7, 2022 5:33 am

KUELEKEA mchezo wa marudiano dhidi ya Club Africain ya Tunisia, uongozi wa Yanga umeibuka na kuweka wazi kuwa mastaa wa timu hiyo wamesikia malalamiko ya mashabiki wao na kuapa kuyachukua kama motisha kuhakikisha wanawashangaza watu kwenye mchezo wa marudiano nchini Tunisia.

Yanga Jumatano wiki hii wakiwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar walilazimishwa suluhu na wageni wao Club Africain katika mchezo wa kwanza wa wa mtoano Kombe la Shirikisho Afrika na kuzua malalamiko makubwa kwa wadau mbalimbali wa soka hususani mashabiki wa Yanga.

Yanga watarudiana na wapinzani wao hao Novemba 9, huu nchini Tunisia, ambapo mshindi wa jumla wa michezo hiyo atafuzu hatua ya makundi.

Msemaji wa Yanga, Ally Kamwe alisema: “Kama taasisi ambayo ina malengo makubwa tumesikitishwa sana na matokeo ambayo tumeyapata juzi Jumatano, wachezaji na viongozi kwa pamoja wamesikia maumivu ya mashabiki na wanachama wetu na kila mmoja ameapa kutimiza wajibu wake kwa asilimia 100 ili kuhakikisha tunapata matokeo yatakayotupeleka makundi nchini Tunisia.

“Tunajua utakuwa mchezo mgumu, lakini tunaamini inawezekana na tutapambana kwa jasho na damu kuhakikisha tunafuzu.”

HUYU HAPA NOVATUS DISMAS MTZ ANAYEWAPAGAWISHA WAZUNGU ULAYA…KAZI YAKE NI BALAAH NA NUSU… YANGA YAWAACHA WAARABU KWENYE MATAA…WAFIKIA MJI WA MBALI KABISA …WATUNISA HAWAAMINI….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply