Home Habari za michezo IMEFICHUKA….HIZI HAPA SABABU NYUMA YA PAZIA WAAMUZI HAWA KUPANGIWA MECHI ZA SIMBA...

IMEFICHUKA….HIZI HAPA SABABU NYUMA YA PAZIA WAAMUZI HAWA KUPANGIWA MECHI ZA SIMBA NA YANGA TU…

Kutumika na kujirudia kwa waamuzi wale wale kwenye mechi za vigogo vya Simba na Yanga vimesababisha kuibuka kwa minong’ono ya chinichini kutoka kwa wadau, lakini Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi nchini, Nassor Hamduni amevunja ukimya kwa kutoa ufafanuzi wa jamabo hilo.

Waamuzi kama Ramadhan Kayoko, Ahmed Arajiga na Elly Sasii ni baadhi ya waamuzi wanaojirudia kila mara kwenye mechi zinazohusu timu hizo kubwa, lakini Hamduni amefafanua kwa nini hali hiyo inatokea.

Hamduni alisema kama kamati wanachozingatia kumteua mwamuzi ni kiwango anachokionyesha na sio upendeleo kama ambavyo wengi wao wamekuwa wakizungumzia suala hilo.

“Duniani kote mwamuzi anateuliwa kutokana na kiwango chake na wala sio vinginevyo, ni kweli kwenye michezo ya Yanga na Simba wamekuwa wakijirudia sana lakini tunapaswa kukubaliana ndio wapo bora,” alisema na kuongeza;

“Tunachoamini tuna waamuzi wazuri ambao kadri ambavyo wanazidi kuchezesha tutawaona tu kwenye hii michezo mikubwa na isitoshe tumeanza kufanya hivyo hivi karibuni ingawa kikubwa ni kuzingatia sheria 17 za soka.”

Katika michezo minane ya Yanga iliyocheza hadi sasa msimu huu, Herry Sasii ndiye kinara akichezesha michezo mitatu na ikishinda yote na alianza dhidi ya Mtibwa Sugar, Ruvu Shooting na ule wa KMC uliopigwa Oktoba 26.

Kwa upande wa Ramadhan Kayoko amechezesha miwili dhidi ya Polisi Tanzania na Simba huku Ahmed Arajiga kutoka Manyara, Raphael Ikambi (Morogoro) na Florentina Zablon wa Dodoma wakichezesha mechi moja kila mmoja wao.

Kwa Simba mwamuzi anayeongoza kuichezesha ni Kayoko ambaye katika michezo minane iliyocheza timu hiyo ameichezesha minne akianza na KMC, Dodoma Jiji, Yanga na Azam FC huku Ahmed Arajiga akichezesha miwili ya Geita Gold na Tanzania Prisons.

Hance Mabena (Tanga) alichezesha na Kagera Sugar huku Tatu Malogo pia wa Tanga akichezesha mechi na Mtibwa Sugar.

SOMA NA HII  UKWELI MCHUNGU....SAKATA LA FEI TOTO LIMEONYESHA TASWIRA HALISI YA YANGA SC...