Home Habari za michezo A-Z YANGA WALIVYOTINGA MAKUNDI CAF KIBABE…MPUNGA WATAKO LIPWA HUU HAPA…

A-Z YANGA WALIVYOTINGA MAKUNDI CAF KIBABE…MPUNGA WATAKO LIPWA HUU HAPA…

Habari za Yanga

Wawakilishi wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho Afrika Yanga imefuzu hatua ya makundi kwenye michuano hiyo baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 ugenini.

Yanga ilikuwa wageni wa Club Africain kutokea Tunisia na ilikubali kulala kwa bao 1-0, lilifungwa na kiungo mtaalamu Aziz Ki baada ya kupokea pasi nzuri na straika, Fiston Mayele dakika 79.

Ki hakuanza kwenye kikosi cha kwanza aliingia kipindi cha pili na alionekana kuongeza umakini kwa Yanga haswa eneo la kushambulia hadi kupata ushindi huo.

Kutokana na kikosi cha Yanga kilivyoaanza jana, walikuwa wakicheza zaidi kwa nidhamu kwenye maeneo yote hadi kuwabana Club Africain kushindwa kupata hata bao la kuotea.

Pengine matokeo hayo yamekuwa na faida na furaha kwa Yanga kutokana na kupata nafasi ya kwenda hatua ya makundi kwenye michuano hiyo.

Inaelezwa wachezaji wa Yanga baada ya kutinga hatua ya makundi mifuko yao itajazwa minoti baada ya kupewa ahadi si chini ya Sh200 milioni kama bonansi ya ushindi.

Yanga inatinga hatua ya makundi kwenye kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuomdolewa Ligi ya mabingwa Afrika na miamba ya soka ya Sudan, Al Hilal.

Mechi ya kwanza Yanga ikiwa nyumbani dhidi ya Club Africain ilitoka suluhu Uwanja Benjamin Mkapa na imekwenda kupata matokeo ya ushindi Tunisia.

YANGA KUJAZWA MANOTI

Yanga baada ya kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika itapata Dola za Kimarekani 275,000 zaidi ya Sh 500 milioni.

Yanga itapata mkwanja huo kutoka Shirikisho la soka Afrika (CAF) kama pesa ya sehemu ya maandalizi baada ya kutinga hatua ya makundi.

Yanga inaenda hatua ya makundi ya mashindano hayo baada ya kufanya hivyo mara ya mwisho 2018.

SOMA NA HII  MWAIKIMBA ASIMULIA ALIVYOLAMBA MILIONI 58 ZA M-BET TANZANIA KIULAINII...KITAMBULISHO CHA NIDA KILIMCHELEWESHA...

1 COMMENT

  1. Huu na hii ni muda wa kumwambia Mr Faustine ,ingependeza kama mngetumia muda mwingi kuchambua au kuandaa makara zinazohusu perfomance ya mpira kama nchi kwanini hatufanikiwi upande wa Taifa Stars mkazungumzia sera ya serikali kuhusu michezo,Lakini ninyi mmejikita kwenye fitna za Simba na Yanga na zaidi mmechukua nafasi ya friends of Simba ,kifupi mnatukwaza,yu spend muda unachunguza madhaifu tena ya conflict,but we have a huge National no Conflict na Wanaume 31M tunashindwa kupata cream ya wachezaji wakucheza hata 100 wa NATIONAL TEAM,na bado mnakaa kusifia eti Simba wanauzoefu ki Mataifa,sasa hizo kamati na almost wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF ni SIMBA FANS mbona upnde wa National Team hawasaidii instead you invest and spend your energy and carolize on how to beat and demolish yanga success.WANACHOJUA NI BRIBERY KWA REFEREES tunajua.
    s t kwenye ku weaken Yanga