Home Habari za michezo PAMOJA NA KUIPELEKA YANGA MAKUNDI CAF…NABI APATA WENGE NA KIKOSI CHAKE..

PAMOJA NA KUIPELEKA YANGA MAKUNDI CAF…NABI APATA WENGE NA KIKOSI CHAKE..

Habari za Yanga

Yanga jana iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Singida Big Stars na kuboresha rekodi yake ya kibabe ya kucheza mechi 47 mfululizo za Ligi Kuu Bara bila ya kupoteza, lakini kuna mkwara mzito kocha, Nasreddine Nabi ameushusha kuanzia mechi hii.

Alichowaambia Nabi wachezaji wake wote kuwa kunaweza kuwa na usajili wa nyongeza katika dirisha dogo la usajili lakini kama kuna staa hajaonyesha kitu kujihakikishia kubaki basi anatakiwa kumshawishi sasa.

Nabi alisema kutokana na ukaribu wa mechi atakuwa anatoa nafasi ya kutosha kwa wachezaji wake karibu wote watakaotangulia kumshawishi mazoezini, akitaka kila mchezaji wake kujitetea.

“Tupo kwenye klabu ambayo ina malengo makubwa, ukiangalia mechi nazo ziko karibu sana ni lazima tuwe na mzunguko wa matumizi ya wachezaji,” alisema Nabi ambaye ameiongoza Yanga kushinda mechi 47 za ndani bila kupoteza.

“Hii ni nafasi kwa kila mchezaji kujiandaa kuanzia mazoezini ili waonyeshe thamani yao kwanini wako hapa, tunaweza kuwa na usajili mdogo tukiona inafaa.

“Hakuna ambaye yuko salama hapa kama kuna malengo hayafikiwi, hii sio kwa wachezaji pekee hata sisi makocha ni wakati wa kila mmoja wetu kuamua kutoa kile klabu inachotarajia.

Aidha, Nabi aliongeza kuwa kuelekea mechi za hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho wanahitaji kuwa na kikosi chenye watu wenye ushindani mkubwa ili kufanya vizuri kwenye mechi hizo zitakazoanza mapema mwakani.

“Nilisema mapema ni lazima tuwe na ubora wa kikosi huko hatua ya makundi mambo yatakuwa magumu zaidi ni vyema tukajitazama sasa na kutafuta ubora wa hizo mechi.

“Ukiziangalia timu ambazo zimeingia makundi utaona jinsi ambavyo tunatakiwa kujiandaa vyema kabla hatujajua tunakutana na timu ipi.”

Yanga inasubiri kujua itapangwa na timu zipi CAF.

SOMA NA HII  MORRISON ALIVURUGA SIMBA...ISHU YAKE YA KURUDI TENA YANGA IKO HIVI KUMBE..AFUNGUKA HILI...