Home Habari za michezo RASMI…TANZANIA KUANDAA AFCON ZOTE MBILI…TFF WAFUNGUKA A-Z MCHAKATO ULIVYO…

RASMI…TANZANIA KUANDAA AFCON ZOTE MBILI…TFF WAFUNGUKA A-Z MCHAKATO ULIVYO…

CAIRO, EGYPT - JULY 19: Algerian team celebrate championship with trophy after the 2019 Africa Cup of Nations final match between Senegal and Algeria at the Cairo Stadium in Cairo, Egypt on July 19, 2019. Algeria won their first Africa Cup of Nations (AFCON) title in 29 years, beating Senegal 1-0 late Friday in Egypt. (Photo by Fared Kotb/Anadolu Agency/Getty Images)

Tanzania imedhamiria kuandaa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa wanaume itakayofanyika mwaka 2027 na ile ya wanawake ya mwaka 2026 na imeanza mikakati mapema ya kuboresha viwanja vilivyopo ili ikidhi vigezo vinavyohitajika.

Hayo yalielezwa juzi na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia katika mkutano mkuu wa 17 wa kawaida wa shirikisho hilo uliofanyika jijini hapa, huku akisisitiza ili kufikia azma hiyo, wataendelea kufungia viwanja visivyokidhi viwango ili vitunzwe na kuboreshwa muda wote.

Karia aliipongeza Serikali kwa kuonyesha nia ya kuvikarabati baadhi ya viwanja nchini kwa kuviwekea nyasi bandia kupitia bajeti ya fedha ya mwaka 2022/2023 ili lengo la kuwa mwenyeji wa mashindano hayo makubwa barani Afrika litimizwe.

Alisema kwa upande wa AFCON ya wanawake itakayofanyika mwaka 2026 Tanzania inajipanga kuandaa peke yake huku ile ya wanaume ya mwaka 2027 ikifikiria kuandaa kwa kushirikiana na majirani zake Kenya na Uganda.

“Viwanja tutaendelea kuvifungia japo watu wanalalamika, matunzo ya viwanja ni pamoja na udhibiti wa matumizi yake, tunapofunga tunatoa somo na elimu, kwa hiyo tutaendelea kudhibiti tushirikiane kufanya hivyo.”

“Hatutasita kufanya hivyo kwa sababu uwanja ukiwa mbovu unaleta athari kwa maisha ya wachezaji na inatuletea picha mbaya huko nje kwa sababu mechi zetu zinaonekana sehemu nyingi, naomba tushirikiane azma yetu iweze kufanikiwa,” alisema Karia.

Akizungumzia mradi wa kituo cha michezo cha Kigamboni alisema kitaanza kutumika kuanzia Januari mwakani na baadhi ya ofisi za shirikisho hilo zitahamia huko huku kambi za timu ya taifa nazo zikiandaliwa hapo.

Vituo hivi vitasaidia kwa mafunzo na kuweka kambi za timu za taifa, ofisi za TFF zitahamia kwa muda Kigamboni na baadhi ya shughuli zetu zitahamia Tanga miradi yetu ikikamilika,” alisema.

SOMA NA HII  KOCHA WA YANGA AHUSISHWA NA NAMUNGO, ISHU IKO HIVI