Habari za michezo

INFANTINO:- KAMA POMBE NI MUHIMU KULIKO KOMBE LA DUNIA…NAWAACHIA FIFA YENU…

admin November 20, 2022 6:34 am

Rais wa FIFA, Gianni Infantino amesema kama pombe ndilo suala kubwa linalopigiwa kelele kuelekea Kombe la Dunia basi atajiuzulu mara moja na kwenda ufukweni kupumzika.

Infatino amesema kutokuwepo kwa pombe viwanjani kwenye michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kuanza leo huko Qatar ni jambo jema tu.

“Usipokunywa bia kwa masaa mawili matatu, unaweza kuishi kuna nchi nyingi zinapiga vita pombe viwanjani ikiwemo Ufaransa.”amesema Infantino.

Hatua hiyo inakuja baada ya Serikali ya Qatar kupiga marufuku uuzaji wa vinywaji hivyo maeneo yanayozunguka viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo.

BAADA YA KUANZA KUTUPIA KAMA ‘JINI’…..MBOMBO AJITANGAZIA VITA AZAM FC… MACHAGUO SPESHO MERIDIANBET  YENYE ODDS KUBWA KOMBE LA DUNIA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply