Home Habari za michezo SALAMBA AFUNGUKA A-Z KINACHOMPA MADILI YA KUCHEZA KWA WAARABU…AITAJA SIMBA ….
Anasema maisha yake kiuchumi yamebadilika akiyatofautisha na kabla ya kuanza kucheza nje na akili yake inapanuka kutokana na mazingira ya aina tofauti anayokutana nayo.
Anasema kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kuhamia kwenye nyumba waliomtafutia, baada ya kufikia kwa Himid Mao “Ndio maana nimesema kwamba sijajisikia mpweke, maana nimekaa na Himid na nitahamia nilikotafutiwa nyumba siyo muda mrefu.”
“Nilianza kuonekana na timu za nje baada ya kuanza kuichezea Simba, nilipata ofa nyingi ndipo kwa mara ya kwanza nikaangukia Al Jahra ya Kuwait, pia huko ni kama kulinifunguliwa milango mingine zaidi;