Home Azam FC AKAMINKO APELEKWA SIMBA NA YANGA…APEWA NAMBA KIKOSI CHA KWANZA

AKAMINKO APELEKWA SIMBA NA YANGA…APEWA NAMBA KIKOSI CHA KWANZA

Habari za Michezo

Kiungo James Akaminko ni kama anazigonganisha Simba na Yanga baada ya mastaa wa zamani wa timu hizo kuonyesha wazi wanatamani akacheze katika klabu zao.

Akaminko, raia wa Ghana mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Azam msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Great Olympic ya Ghana.

Starika wa zamani wa Yanga, Moro United na Prisons, Hery Morris alisema Akaminko ni kiungo mshambuliaji mwenye uwezo wa kucheza kama mkabaji jambo linaloifanya Azam iwe salama kwenye eneo la kiungo.

“Huyu anaweza kucheza Yanga kwa sababu kuna wachezaji ambao hawamfikii kwa uwezo na wapo pale. Sio tu kwetu hata timu yoyote ile hapa nyumbani anaweza kucheza. Kiukweli Azam imepata jembe,” alisema Morris.

“Ana uwezo wa kujua mchezaji mwenzake anapita wapi na kupiga pasi. Anakaba sana halafu mpambanaji wa hali ya juu na ndio wachezaji wanaohitajika.”

Straika wa zamani Simba, Emmanuel Gabriel ‘Batgol’ alisema Akaminko ni jembe na anatamani angemuona kwenye kikosi cha Simba.

“Yule ni mchezaji mzuri sana kwa kweli. Anaweza kucheza Simba kabisa. Azam wamepata mchezaji na kama ingekuwa inacheza mashindano ya kimataifa sidhani kama ingeendelea kubaki naye,” alisema Gabriel aliyewahi kukipiga Nazareth ya Njombe.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO YANGA WALIVYOTUMIA 265MIL 'KUNUNUA USHINDI WA MECHI ZAO'...INJIA HERSI AFUNGUKA A-Z....