Home Habari za michezo BAADA YA KUONA MBEYA CITY WAMEWEZA…POLISI TZ WAAMUA KUINGIA NA STAILI HII...

BAADA YA KUONA MBEYA CITY WAMEWEZA…POLISI TZ WAAMUA KUINGIA NA STAILI HII DHIDI YA SIMBA…

UONGOZI wa Polisi Tanzania umetambulisha kampeni yake mpya ya ‘Lazima Utoe Ushirika’ katika michezo yao ya Ligi Kuu Bara watakayochezea kwenye Uwanja wa Ushirika ulioko Moshi mkoani, Kilimanjaro na wataanza kuitekeleza pale watakapoikaribisha Simba kutoka Dar es Salaam, imefahamika.

Maafande hao wataikaribisha Simba katika mechi ya raundi ya 13 ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa keshokutwa kuanzia saa 10:00 jioni.

Polisi Tanzania wanashuka katika dimba la nyumbani kwao Ushirika kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya uwanja huo uliokuwa unakarabatiwa kupata ruhusa kutoka kwenye mamlaka husika inayosimamia Ligi Kuu.

 Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma, alisema ingawa timu yao msimu huu imekuwa na ‘mwendo wa kinyonga’, sasa wanarudi nyumbani na wataitumia vyema kampeni ya “Lazima Utoe Ushirika” kwa kuvuna pointi zote tatu.

Juma alisema wanaanza rasmi ukurasa mpya ndani ya uwanja wao wa asili na wanaimani Wekundu wa Msimbazi hawataondoka na pointi hata moja.

“Japo tuna mwendo wa kinyonga, sasa tunarudi nyumbani, tunarudi nyumbani kwa mashabiki wetu, tumecheza viwanja sita tofauti, sasa tunarudi Ushirika uwanja ambao tunapata matokeo, tuna matumaini makubwa ya kuitekeleza kampeni yetu,” alisema kiongozi huyo.

Aliongeza kampeni hiyo sio kwa ajili ya mechi moja bali wataiendeleza katika kila mechi watakayocheza kwenye dimba la Ushirika.

Baada ya kucheza na Simba, Polisi Tanzania itabakiwa kwenye uwanja huo na kusubiri kuwakaribisha Azam FC katika mechi nyingine ya ligi hiyo itakayofanyika Desemba 6, mwaka huu.

SOMA NA HII  WIKIENDI YA KIBABE HII HAPA....ODDS ZA KUSHIBA ZA MERIDIANBET ZINAKUPA UHAKIKA WA MAMILIONI...