Home Habari za michezo KARIA AZIPIGA MKWARA SIMBA NA YANGA KISA U-20…

KARIA AZIPIGA MKWARA SIMBA NA YANGA KISA U-20…

Katika kukuza soka la vijana na kuzalisha wachezaji wengi wapya watakaolisaidia taifa hapo baadae, Shirikisho la Soka nchini (TFF) limepitisha azimio kuwa kwa sasa timu za vijana chini ya umri wa miaka 17 na 20 (U-17 na U-20) ndizo zitashiriki Ligi za Wilaya (daraja la nne).

Hayo yameelezwa na Rais wa TFF, Wallace Karia katika mkutano mkuu wa 17 wa shirikisho hilo jijini Mwanza huku akisisitiza kuwa wachezaji wote watatakiwa kuwa na vyeti vya kuzaliwa ndipo wasajiliwe kucheza.

Amesema klabu ambayo haitafanya hivyo haitaruhusiwa kushiriki ligi hizo, za mikoa na zile za mabingwa wa mikoa (RCL).

Ameviagiza vyama vya soka vya mikoa kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wake kwa ufanisi kwani ligi nyingi za wilaya na mikoa zimejaa wachezaji wengi ambao wameshacheza madaraja ya juu wakachoka.

“Kwakuwa hatuna ligi za vijana tunataka vijana zaidi kwenye ligi zetu za chini, tunataka Ligi za Wilaya kuchezwa na vijana wasiozidi miaka 20, wilaya zitekeleze hilo na usajili utafanywa kwa wachezaji wenye vyeti vya kuzaliwa wakionyesha umri wao sahihi,” amesema.

“Haya ni maelekezo klabu ambayo haitafanya hivyo haitashiriki Ligi ya Mabingwa wa mikoa, pia tunataka kuboresha Ligi zetu za vijana U-17 na U-20 kwa timu za Ligi Kuu kuanzia msimu ujao zitachezwa nyumbani na ugenini vilabu muondoke hapa mkijua U-20 inayokuja ni home and away,” amesisitiza.

Akizungumzia mashindano mbalimbali yanayoendelea nchini kwa jina maarufu la ‘Ndondo Cup’ ametaka uandaliwe utaratibu maalum ambao hautaathiri Ligi za Wilaya na mikoa.

“Ndondo zisiharibu Ligi za mikoa na wilaya, upangwe utaratibu mzuri ambao hautaharibu kwa sababu tumeona baadhi ya maeneo inaathiri,” amesema Karia.

SOMA NA HII  ISHU YA MORISSON KUSAJILIWA YANGA...SIMBA WAIBUKA NA TAMKO HILI...AHMED ALLY ADAI NI HESHIMA KUBWA KWAO...