Home Habari za michezo PAMOJA NA SIMBA QUEENS KUKOSA KOMBE…OPAH AACHA GUMZO KUBWA MOROCCO…

PAMOJA NA SIMBA QUEENS KUKOSA KOMBE…OPAH AACHA GUMZO KUBWA MOROCCO…

Mfungaji wa bao la timu ya wanawake ya Mamelodi Sundowns, Boitumelo Rabale dhidi ya Simba Queens kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, amemtaja Opah Clement kuwa miongoni mwa wachezaji hatari aliowaona msimu huu kwenye michuano hiyo ambayo imefanyika kwa mara ya pili.

“Tulimwona kabla ya mchezo kuwa ni kati ya wachezaji muhimu kwa Simba (Queens), mpango wetu haukuwa kumzuia, tulijiandaa kuhakikisha anakosa nafasi za kutuletea madhara, ulikuwa mchezo mgumu sana ila tulipambana kama timu na kuingia fainali.

“Wapo wachezaji wengi wazuri ambao nimewaona lakini na yeye ni mmoja kati yao, naamini tutakutana naye tena msimu ujao,” alisema nyota huyo.

Katika fainali hizo, Simba Queens ilishiriki kwa mara ya kwanza na kuweka historia ya kutinga nusu fainali huku Mamelodi wenyewe hii ni mara ya pili ya kwanza ilikuwa msimu uliopita ambapo ilitwaa ubingwa huo.

SOMA NA HII  TUKIO LA MANULA KUTOKWA DAMU MKONONI GHAFLA KABLA YA MECHI YA JANA...ISHU NZIMA KUMBE IKO HIVI...SHABIKI ATAJAWA..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here