Home Habari za michezo KAZE : YANGA KUWA ‘UNBEATEN’ NI FAIDA….KUNA WATU WANATUOGOPA AFRIKA NZIMA..

KAZE : YANGA KUWA ‘UNBEATEN’ NI FAIDA….KUNA WATU WANATUOGOPA AFRIKA NZIMA..

Habari za Michezo Bongo

Kocha Msaidizi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Cedrick Kaze amesema Rekodi ya UNBEATEN haiwapi Presha wao kama wahusika, na badala yake imekua ikiwasaidia kuwapa matokeo katika Michezo inayowakabili.

Young Africans inashikilia Rekodi ya kucheza bila kufungwa ‘UNBEATENA’ tangu msimu uliopita 2021/22, ikicheza michezo 45 ya Ligi Kuu Tanzania, leo Alhamis (Novemba 17) ikitarajia kukutana na Singida Big Stars Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Akuzungumza na Waandishi wa Habari katika Mkutano maalum kuelekea mchezo huo, Kocha Kaze alisema: “Kuwa unbeaten haitupi sisi presha yoyote, sisi tunacheza kwa malengo yetu ya kupata mataji hivyo kila mechi tunahitaji kujiandaa na kushinda. Unaweza kuwa unbeaten na usiwe bingwa hivyo haitakuwa na maana. Hatujiwekei presha kubwa ya unbeaten tunacheza kwa malengo”

“Yanga SC ni timu kubwa, tunawaheshimu wapinzani wetu lakini naamini timu nyingi zinatuhofia sisi. Haijalishi tunacheza wakati gani na eneo gani lakini najua timu nyingi zinacheza kwa tahadhari kubwa kwa sababu wanajua ukubwa wetu”

“Mechi yetu na Singida big Stars ni mchezo mgumu kutokana na ukubwa wa kikosi cha Singida hasa ukizingatia mwalimu waliye nae (Hans) ni mzoefu sana na amewahi kuitumikia Yanga SC kwa mafanikio”

SOMA NA HII  ISHIKILIE SLOT YA THIRSTY VIKING KWENYE MERIDIANBET CASINO KWA UHAKIKA WA MAOKOTO...