Home Habari za michezo MANARA ASHTUSHWA NA KIWANGO CHA DIARRA…AMMIMINIA ‘POVU’ KAMA LOTEE…

MANARA ASHTUSHWA NA KIWANGO CHA DIARRA…AMMIMINIA ‘POVU’ KAMA LOTEE…

Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amemmwagia sifa kipa wa timu hiyo, Djigui Diarra raia wa Mali ambaye ameonyesha kiwango cha hali ya juu kwa siku za hivi karibu.

Kauli hiyo ya Manara inakuja baada Diarra kuisaidia timu yake kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mbali na hilo, Diarra alifanya kazi kubwa kwenye mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar katika Dimba la CCM Kirumba Mwanza na huku akipangua mkwaju wa penati.

“Ni kweli tuna makipa bora sana kwenye Ligi kuu yetu ila kuwafananiaha Makipa wetu na Diarra ni kujitafutia dhambi kama za kuzini tu.

“Huyu hadaki tu kizamani kama Watangazaji wetu wa wakati ule walivyokuwa wakitangaza, kadaka kama Nyani.

“Huyu ni kipa wa kisasa, anafanya saves, ile kurukia mpira kama Nyani ni uzamani, kazi ya kipa wa kileo ni kuzuia lango lake mpira usingie, sio kuruka ruka hovyo.

“Kisha anawazidi wote chini, yeye ni Sweeper kisha Boll Control yake ni ya makipa wa hadhi ya kidunia, anaanzisha mwenyewe mashambulizi, tena sio Kwa kurusha ili kuwahi counter attacks, anapasia kwa Miguu yake.

“Kubwa ni Commanding Goalkeeper, ni kiongozi ndani ya Uwanja, Kiukweli ubora wake ni mkubwa kuliko maradufu ya wenzake, kawaacha mbali mno. Yeye yupo Makka wenzake wapo Nantumbo,” amesema Manara.

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO...AZAM FC NAO HAWATAKI MZAHA AISEE...WAMSHUSHA BONGO KOCHA WA SEVILLA YA HISPANIA..