Home Habari za michezo MGUNDA: LEO ‘TUTAWATEMBEZEA MOTO’ USIOZIMIKA POLISI TZ….

MGUNDA: LEO ‘TUTAWATEMBEZEA MOTO’ USIOZIMIKA POLISI TZ….

Kocha Msaidizi Simba SC
[the_ad id="25893"]

Kocha mkuu wa klabu ya Simba Juma Mgunda ameongea na wanahabari jana kuelekea mchezo wao dhidi ya klabu Polisi Tanzania na kueleza mipango yake kuelekea mchezo huo ni kupata alama tatu muhimu katika mchezo huo.

Kocha huyo anaeleza “Maandalizi ya mchezo yamekamilika na wachezaji wapo kwenye hali nzuri,Tunajua mechi itakua ngumu. Na Polisi haipo kwenye nafasi nzuri tutaiheshimu lakini malengo yetu ni kupata alama tatu. Klabu ya Simba itahitaji kupata matokeo mazuri katika mchezo huo ili iweze kukaa kileleni kwa mwa msimamo.

Mchezo wa Simba na Polisi Tanzania ambao unatarajiwa kupigwa katika dimba la Ushirika mkoani Kilimanjaro majira ya saa kumi kamili jioni.

Klabu ya Polisi Tanzania haipo kwenye kiwango kizuri kwasasa hivo nao wanatarajia kutoa ushindani mkali hapo kesho ili waweze kujinasua kwenye nafasi ya 15 na alama zao 9 tu.

Simba wao wametoka kudondosha alama dhidi ya Mbeya City mchezo uliomalizika huko jijini Mbeya hivo watakua wanahitaji alama tatu muhimu ili kuendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kugombania Ubingwa wa ligi kuu ya NBC msimu huu baada ya kuukosa msimu uliomalizka.

Swali ambalo wadau wanaendelea kujiuliza je Simba wataendelea na rekodi yao mbovu ya kuteseka katika viwanja vya mkoani kwani msimu huu wakiwa wamefanikiwa kupata alama tatu tu kwenye viwanja vya mkoani.

SOMA NA HII  MIGOLI YA BOCCO NDANI YA SIMBA SC YAMTIA WAZIMU MAYELE...HATARI YAKE IKO HAPA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here