Home Habari za michezo WORLD CUP: ALIYESHANGILIA KAMA RONALDO MBELE YAKE AFUNGUKA SABABU YA KUFANYA HIVYO..

WORLD CUP: ALIYESHANGILIA KAMA RONALDO MBELE YAKE AFUNGUKA SABABU YA KUFANYA HIVYO..

Mshambulizi wa Ghana Osman Bukari anasema hakumdharau Cristiano Ronaldo alipoigiza shangwe ya bao la nyota huyo wa Ureno baada ya kufunga bao dhidi yao kwenye mechi ya Kundi H ya Kombe la Dunia siku ya Alhamisi.

Bukari aliyeingia kama mchezaji wa ziada alifunga goli na kufanya matokeo kuwa 3-2 katika dakika ya 89 kabla ya kukimbia kuelekea kwenye kibendera cha kona na kuigiza pozi la Ronaldo almaarufu ‘Siu’.

Fowadi huyo wa zamani wa Manchester United alikuwa ameipa Ureno bao la kwanza bao muhimu sana kwenye Uwanja wa 974 mjini Doha lakini akatolewa wakati Bukari alipofunga kwa kichwa kutoka umbali wa yadi sita.

“Nimegundua kusherehekea kwangu kumezua maoni yanayodai sikumheshimu Ronaldo,” mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alichapisha kwenye Twitter.

“Hii si sahihi. Nilizidiwa na hisia za wakati wa kuifungia nchi yangu bao kwenye mechi yangu ya kwanza ya Kombe la Dunia na kusababisha kushangilia kwangu.

“Malezi yangu hayaniruhusu kuwakosea heshima watu wazima na hususan watu ninaowatumia kama kioo .”

Mabingwa hao wa Ulaya wa 2016 walifanikiwa kupata ushindi huo, na kuiacha Ghana mkiani mwa kundi kufuatia awamu ya kwanza ya mechi baada ya Uruguay na Korea Kusini kutoka sare ya 0-0 mapema Alhamisi.

Ronaldo amekuwa mtu wa kwanza kufunga katika michuano mitano tofauti ya Fifa ya Kombe la Dunia alipoifungia Ureno kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 65 kufuatia mpira uliopigwa na Mohammed Salisu.

Kocha wa Black Stars, Otto Addo hakufurahishwa na mwamuzi Ismail Elfath.

“Nadhani ulikuwa uamuzi mbaya sana, tulikuwa tunacheza mpira. Sijui kwanini VAR (Video Assistant Referee) haikutumika, hakukuwa na maelezo yoyote,” alisema Addo.

“Ulikuwa uamuzi mbaya. Kwa hakika ulikuwa ni fauli dhidi yetu.”

Addo alisema alijaribu kuzungumza na mwamuzi kuhusu baadhi ya maamuzi baada ya mechi.

β€œNilitaka kufanya hivyo kwa utulivu lakini niliambiwa yuko kwenye kikao, hakutupenda kabisa , tulipata kadi chache za njano ambazo zilistahili lakini pia kulikuwa na kuvutwa kwa jezi na kusimamisha mashambulizi ya kujibu , pia makosa yaliohitaji kadi za njano lakini hawakupewa.”

Alipoulizwa kuhusu bao muhimu la Ronaldo, Addo alisema: “Ikiwa mtu atafunga bao, hongera. Lakini hii lilikuwa zawadi, zawadi kweli.”

Beki wa ingi ya kulia wa Brighton, Tariq Lamptey pia aliingia kama mchezaji wa akiba wa kipindi cha pili na kusema mechi yake ya kwanza ya fainali za Kombe la Dunia ilikuwa ya “uchungu” mwingi.

“Ni vigumu. Siku nyingine tunapata matokeo tofauti,” aliongeza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.

“Siku zote tulijiamini na tuliamini kuwa tunaweza kupata matokeo mazuri.

“Lazima tutimue vumbi sasa, tufanye kazi kwa bidii katika mazoezi na kusubiri mechi inayofuata.”

Ghana watacheza na Korea Kusini katika mechi yao ya pili ya Kundi H siku ya Jumatatu na mchezo wao wa mwisho dhidi ya Uruguay mnamo Ijumaa, 2 Desemba.

SOMA NA HII  KUHUSU TETESI ZA MASTAA SIMBA KUKIMBIA..AHMED ALLY AVUNJA UKIMYA...AANIKA HALI ILIVYO..