Home Habari za michezo FT:YANGA SC 2-0 MBEYA CITY…..MAYELE AFANYA KILICHOMSHINDA BOCCO…YANGA KAMA ARSENAL TU…

FT:YANGA SC 2-0 MBEYA CITY…..MAYELE AFANYA KILICHOMSHINDA BOCCO…YANGA KAMA ARSENAL TU…

KLABU ya Yanga imeendelea kujiweka vizuri kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara mara baada ya kufanikiwa kuichapa Mbeya City mabao 2-0 na kuwafanya kufika pointi 32 akiwa ameshuka dimbani mara 12.

Fiston Kalala Mayele ameendelea kutikisa nyavu baada ya leo tena kupachika mabao mawili na kumfanya aendelea kushikilia usukani kwa wapachikaji wa mabao ndani ya ligi kuu akifikisha mabao 10.

Bao la kwanza Mayele alifunga dakika 24 ya mchezo kipindi cha kwanza na bao la pili akifunga dakika 79 kipindi cha pili.

Kwa matokeo haya Yanga SC imefikisha mechi 49 za Ligi Kuu bila kupoteza , rekodi ambayo kwa pale Uingereza inashikiliwa na klabu ya Arsenal.

SOMA NA HII  HUU HAPA 'UCHAWI' WA AZIZI KI KUWA MOTO MSIMU HUU NDANI YA YANGA....BALAA LAKE SIO POA..