Home Habari za michezo BAADA YA KUWATANDIKA BAKORA TZ PRISONS JANA….YANGA WAIFUATA NAMUNGO ‘ASUBUHI ASUBUHI’…

BAADA YA KUWATANDIKA BAKORA TZ PRISONS JANA….YANGA WAIFUATA NAMUNGO ‘ASUBUHI ASUBUHI’…

Habari za Yanga

MSAFARA wa wachezaji 21 wa Yanga umesafiri saa 11:00 alfajiri ya leo kuelekea mkoani Lindi, kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo.

Kwa kutumia shirika la ndege la Precision, msafara huo utatua uwanja wa ndege wa Mtwara kisha kuunga kwa basi kuelekea Ruangwa, Lindi.

Wachezaji walioambatana na timu ni pamoja na Djigui Diarra, David Bryson, Erick Johola, Kibwana Shomary, Joyce Lomalisa, Djuma Shabani, Ibrahim Abdullah, Dickson Job, Yanick Bangala, Khalid Aucho, Gael Bigirimana, Zawadi Mauya, Jesus Moloko, Tuisila Kisinda, Denis Nkane, Clement Mzize, Aziz Ki, Bernard Morrison, Fiston Mayele, Dickson Ambundo na Feisal Salum.

Kiungo Salum Abubakari na winga Farid Mussa watakosekana kwenye mchezo huo kwa sababu ya majeraha.

SOMA NA HII  LIPANGILE WA KMC AMFUTA MACHOZI MJANE MWENYE WATOTO 19 KUPITIA MERIDIANBET...