Home Habari za michezo FT: NAMUNGO 0-2 YANGA SC….KISINDA KAONA MWEZI…BANGALA KAMA MAYELE TU…

FT: NAMUNGO 0-2 YANGA SC….KISINDA KAONA MWEZI…BANGALA KAMA MAYELE TU…

NGOMA imekamilika Uwanja wa Majaliwa ubao ukisoma Namungo 0-2 Yanga ambapo wenyeji wamekwama kutamba mbele ya wageni.

Namungo walizidiwa ujanja kipindi cha kwanza kutokana na makosa ya kipa Jonathan Nahimana kwenye kuokoa pigo la faulo ya Aziz KI iliyokutana na Yannick Bangala dakika ya 40.

Bao la pili, Nahimana katika harakati za kuokoa shuti la Tuisila Kisinda alikutana nalo likiwa limezama ndani ya neti dakika ya 82.

Ni bao la kwanza kwa Kisinda baada ya kurejea ndani ya Yanga msimu wa 2022/23.

Namungo walikuwa kwenye kasi ya kusaka bao kipindi cha pili lakini shuti lao moja ambalo lililenga lango kupitia kwa Relliats Lusajo liliokolewa na Diarra Djigui.

Sasa Yanga inakamilisha mzunguko wa kwanza ikiwa na pointi 38 nafasi ya kwanza.

SOMA NA HII  SIKIZA...KILA UNAPUA ZOMBI MERIDIANBET WANAKULIPA KUPITIA CASINO YAO YA ZOMBIE APOCALYPSE...