Fei toto Yanga SC
Azam FC

AZAM WAPANIA KWA FEI TOTO…WAMWEKEA MIL 350 MEZANI PAMOJA NA MSHAHARA WA MIL 10 KWA MWEZI..

admin December 8, 2022 2:02 pm

Kiungo wa Yanga SC, Feisal Salum (Fei Toto) huenda akatimkia kunako klabu ya Azam mwisho mwa msimu huu (2022/23) baada ya Azam kumuwekea mezani takribani Tsh. Milioni 350 kama pesa ya usajili.

Katika kuhakikisha wanainasa saini ya kiungo huyo Azam wapo tayari kutanguliza kishika uchumba ambapo kila mwezi Fei Toto atapokea Milioni 10 hadi dirisha kubwa la usajili litakapo funguliwa na kumwaga wino rasmi kuwatumikia matajiri hao wa jiji la Dar es Salaam.

Inasemekana Azam wamekubali kuuvunja mkataba wa Fei na Yanga ambapo watalipa milioni 100 na mshahara wa miezi mitatu kama masharti yaliyopo kwenye mkataba wake na Yanga.

TAKUKURU WASHIKILIA FAILI LA SIMBA….MGUNDA KAWAPITISHA HAWA DIRISHA DOGO… TETESI : KOCHA WA AL AHLY KUTUA SIMBA SC…MPANGO MZIMA UKO NAMNA HII…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply