Home Habari za michezo HIVI NDIVYO MAYELE ALIVYOMBURUZA MOSES PHIRI KITAKWIMU…NTIBAZONKIZA HOI BIN TAABANI..

HIVI NDIVYO MAYELE ALIVYOMBURUZA MOSES PHIRI KITAKWIMU…NTIBAZONKIZA HOI BIN TAABANI..

Habari za Simba

Mshambuliaji wa klabu ya Young Africans SC, Fiston Mayele amechaguliwa kuwa Mchezaji bora wa mwezi Novemba wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/23 akiwashinda Mosses Phiri wa Simba na Saido Ntibazonkíza wa Geita Gold alioingia nao fainali.

Katika mwezi Novemba Mayele alionesha kiwango kizuri baada ya kutoa mchango mkubwa kwa Yanga, ikiwa ni pamoja na kufunga mabao saba, kati ya mabao hayo matatu ‘hat trick’ akifunga katika mchezo mmoja.

Yanga ndio timu iliyopo kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 38.

SOMA NA HII  BAADA YA KUANZA KUTUPIA SIMBA...OKRAH ATOA UJUMBE HUU KWA MASHABIKI NA KWA KOCHA MPYA....