
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Adenor Leonardo Bacchi maarufu kwa jina la Tite rasmi ameachia ngazi kukinoa Kikosi cha timu hiyo baada ya kutupwa nje ya Michuano ya Kombe la Dunia 2022 katika hatua ya Robo Fainali dhidi ya Croatia.
Kocha Tite amechukua maamuzi hayo baada ya kutupwa nje ya Michuano hiyo mikubwa duniani inayoendelea nchini Qatar, Kocha huyo raia wa Brazil alichukua majukumu ya kukinoa Kikosi hicho mwaka 2016.
Michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Russia, timu hiyo ya taifa ya Brazil ilicheza Michuano hiyo na kuishia hatua ya Robo Fainali baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Ubelgiji.
Licha ya kuwa na kizazi maarufu kwa sasa ulimwenguni, kina Neymar Jr, Richarlison, Rafinha, Vinicius Jr na wengine, Brazil wameshindwa kutamba katika Michuano hiyo na kutupwa nje na Croatia katika hatua hiyo ya Robo Fainali kwa changamoto ya mikwaju ya Penalti 4-2, baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 120’ za mchezo huo.
Je? Brazil watamtangaza nani kuwa Kocha Mkuu wa Kikosi chao baada ya Kocha Tite kuondoka.
SOMA NA HII TAIFA STARS KUPASHANA NA MISRI YA KINA SALAH KABLA YA AFCON....RATIBA KAMILI HII HAPA...