Habari za michezo

BAADA YA KUTUPWA NNJE KOMBE LA DUNIA…KOCHA WA BRAZIL KAONA ISIWE KESI…KAWASUSI TIMU YAO HUKO…

admin December 10, 2022 10:51 am

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Adenor Leonardo Bacchi maarufu kwa jina la Tite rasmi ameachia ngazi kukinoa Kikosi cha timu hiyo baada ya kutupwa nje ya Michuano ya Kombe la Dunia 2022 katika hatua ya Robo Fainali dhidi ya Croatia.

Kocha Tite amechukua maamuzi hayo baada ya kutupwa nje ya Michuano hiyo mikubwa duniani inayoendelea nchini Qatar, Kocha huyo raia wa Brazil alichukua majukumu ya kukinoa Kikosi hicho mwaka 2016.

Michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Russia, timu hiyo ya taifa ya Brazil ilicheza Michuano hiyo na kuishia hatua ya Robo Fainali baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Ubelgiji.

Licha ya kuwa na kizazi maarufu kwa sasa ulimwenguni, kina Neymar Jr, Richarlison, Rafinha, Vinicius Jr na wengine, Brazil wameshindwa kutamba katika Michuano hiyo na kutupwa nje na Croatia katika hatua hiyo ya Robo Fainali kwa changamoto ya mikwaju ya Penalti 4-2, baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 120’ za mchezo huo.

Je? Brazil watamtangaza nani kuwa Kocha Mkuu wa Kikosi chao baada ya Kocha Tite kuondoka.

TAKWIMU…MZUNGUKO UJAO TARAJIA MAGOLI ZAIDI…HISTORIA ITAANDIKWA BONGO… WAKATI MAMBO YAKIZIDI KURINDIMA QATAR… HIVI NDIVYO TANAPA WANAVYOENDELEA KUIPAISHA TZ

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply