Home Habari za michezo PAMOJA YA KUPITIA MAMBO MAZITO MSIMBAZI…OKWA APATA WA KUMTETEA KIBABE…

PAMOJA YA KUPITIA MAMBO MAZITO MSIMBAZI…OKWA APATA WA KUMTETEA KIBABE…

Nelson Okwa akiwa Simba SC

Nelson Okwa, nyota aliyesaliwa Simba kutoka Nigeria na kushindwa kukuna nyoyo za mashabiki wa timu hiyo, amepata mtetezi baada ya kipa wa Rivers United, Victor Sochima kumkingia kifua kwa kuwataka viongozi na benchi la ufundi kumpa muda ili waupate utamu wa mshambuliaji huyo.

Sochima mwenye umri wa miaka 23, aliyecheza kikosi kimoja na Okwa walipokuwa wote Rivers Utd ya kwao Nigeria alisema muda mwingine mchezaji anaweza kushindwa kuonyesha makali mapema kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utofauti wa mazingira na hata kuandamwa na majeraha.

Lakini hayo, alisema hayapaswi kutumika kama kigezo cha mchezaji kujitetea;”Najua (Nelson) ni mmoja kati ya wachezaji ambao kila mtu alikuwa akimuongelea, ni hodari na mapambanaji, sio mwepesi wa kukata tamaa, ni kiongozi.

“Sijajua shida ni nini hasa lakini nadhani mazingira na majeraha ambayo nilisikia amekumbana nayo vimemuondoa kwenye mstari, ila anapaswa kupewa muda anaweza kuisaidia Simba kutokana na ubora ambao yupo nao, ni mchezaji wa kiwango cha juu.”

Wiki chache zilizopita Nelson alikuwa kwao, Nigeria ambako alikuwa akifanya matatibabu ya nyama za paja ambazo zilikuwa zikimsumbua na sasa yupo sawa amejumuika na kikosi cha kwanza cha Juma Mgunda kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Geita Gold.

Katika mahojiano yake ya mwisho na gazeti hili ana kwa ana, Okwa alisema, “Moyoni kwangu nina deni kubwa natakiwa kulilipa kwa mashabiki wa Simba kwani wameweka imani kubwa kwangu kwa kuamini naweza kufanya vitu vingi bora kwenye mechi za mashindano mbalimbali,

“Hakuna njia nyingine ya kulipa deni hilo bali natakiwa kurejea uwanjani kwa nguvu kuhakikisha napata nafasi ya kucheza na kutoa mchango kwa timu kufanya vizuri kwa kuonyesha kiwango bora. Ubora wa mchezaji unaonekana pale kwenye kutimiza majukumu ya nafasi yake kwenye michezo mfululizo.”

Okwa aliyekuwa nahodha wa Rivers aliwakosha mabosi wa Simba baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

SOMA NA HII  KISA MAZOEZI YA YANGA..AUCHO ASHINDWA KUJIZUIA...AWACHANA WACHEZAJI WENZAKE..NABI ASHANGAA TU...