Habari za michezo

TRY AGAIN: KUJIUZULU KWA BARBARA NI UPEPO MBAYA…SIMBA NI TIMU KUBWA AFRIKA…

admin December 12, 2022 9:03 pm

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba SC Salim Abdallah ‘Try Again’ ametuliza hali ya hewa ndani ya Klabu hiyo, baada ya aliyekua Afisa Mtendaji Mkuu ‘CEO’ Barbara Gonzalez kutangaza kujiuzulu.

Barbara akithibitisha kujiuzulu juzi Jumamosi (Desemba 10), na kuzua taharuki kwa Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo ambao walihoji maswali mengi katika Mitandao ya Kijamii kuhusu kuondoka kwa kiongozi huyo.

Tyr Again amesema kuondoka kwa Barbara hakutaharibu lolote ndani ya Klabu hiyo na badala yake mazuri yoteyataendelezwa na kufikiwa kwa lengo linalokusudiwa msimu huu 2022/23.

“Simba ni Klabu kubwa haitabadilika eti kwa sababu CEO ameamua kujiuzulu nafasi yake, Simba itaendelea kuwepo na kufanikisha mipango yake kwa sababu ina uongozi unaofahamu dira yake.

Simba SC ni Klabu kubwa Barani Afrika, hiki kilichotokea ni upepo mbaya ambao ni kawaida kupitia popote pale, lakini niwahakikishiea Wanachama Klabu yao ipo salama na itaendelea na mipango yake kama kawaida,” amesema Try Again.

Amesema kwa sasa wapo katika mikakati ya kuiandaa timu yao kuelekea hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika lakini pia wanaendelea na mchakato wa kuimarisha kikosi kwenye Dirisha Dogo, ili kiweze kufanya vizuri katika Michuano wanayoshiriki msimu huu.

TETESI…BAADA YA SIMBA NA YANGA KUMSUSA….WACONGO WAMVUTA GEORGE MPOLE KWAO… NDOA YA MBRAZILI NA SINGIDA BIG STARS YAOTA MBAWA…YALIYONYUMA YA PAZIA HAYA HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply