Habari za simba
Habari za michezo

KABURU ACHOKUA FOMU ZA KUGOMBEA UBOSI SIMBA…VIGOGO WENGINE HAWA HAPA…

admin December 13, 2022 7:53 am

Wagombea 13 wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba SC utakaofanyika Januari 29, mwakani.

Kati ya wagombea hao wanne wanawania nafasi ya mwenyekiti na tisa nafasi ya Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.

Miongoni mwa waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti ni aliyekuwa Mtunza Fedha wa klabu hiyo, Yusuph Nassor Majid ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS).

Wengine wanaowania ni Makamu Mwenyekiti wa zamani Geofrey Nyange ‘Kaburu’ Yusuph Omar Yenga, na Eng. Rashid Khamsini.

Katika nafasi ya Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi mpaka sasa waliochukua fomu ni wagombea tisa.

Wagombea hao ni Iddy Noor Kajuna, Abubakar Zebo, Eng. Rashid Khamsini, Hawa Subira Mwaifunga, Laurian Mganga, Elisony Edward Mweladzi, Lameck Lawrance na Abdallah Rashid Mgomba.

Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu litafungwa rasmi Disemba 19, mwaka huu.

DILI LA MAZNOKI  LAFIKIA PATAMU SIMBA….MGUNDA AKABIDHI MAJINA YA VIFAA VIPYAA… TUONGEE KIMPIRA…HI ISHU YA BARBARA KUJIUZULU SIO KUBWA KIVILEE..ILA BADO KUNA TATIZO SIMBA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply