Home Habari za michezo MWAKINYO: WAZANZIBAR HAWATUTAKI…HUU MUUNGANO UNAUNGANISHA NINI..?

MWAKINYO: WAZANZIBAR HAWATUTAKI…HUU MUUNGANO UNAUNGANISHA NINI..?

Hassan Mwakinyo

Bondia Hassan Mwakinyo (27) @_hassanmwakinyojr ambaye anajiandaa na pambano lake dhidi ya Bondia Mmarekani Peter Dobson (32) ambalo limepangwa kufanyika Desemba 30, 2022 katika Uwanja wa Mao Tse Tung, Zanzibar, ameelezea masikitiko yake kwa kile alichodai Mabondia wa Zanzibar wameandika barua wakidai hiyo ni fursa ya Wazanzibar na sio ya Watanzania Bara.

Pambano hilo la Mwakinyo vs Mmarekani Dobson ni la kugombania mkanda wa WBC International Super Welter.

Mwakinyo amesema “Baada ya miaka mingi kupita nimekuwa mstari wa mbele sana kuipambania Boxing ya Zanzibar mpaka kufanikiwa kupata ridhaa kupitia Mh. Rais wa Zanzibar na Baraza lake kupata kibali cha kufanya fight.

“Ajabu ni kwamba Boxer wa Zanzibar wasioona ukubwa wa hili jambo wameandika barua wakidai ile ni fursa yao Wazanzibar na sio ya Watu wa Tanzania Bara so hawataki tujihusishe nao”

“Na sasa sijui ikisemwa kuwa kuna Muungano uliopo kati yetu Muungano huo unaunganisha kitu gani anyway kila la kheri Mabingwa.”

SOMA NA HII  A-Z JINSI SIMBA ILIVYOIFINYANGA RUVU SHOOTING JANA...BOCCO ATOA GUNDU LA MIEZI TISA...

1 COMMENT

  1. Walichoongea mabondia wa Zanzibar ni sahihi kabisa kwa nini fursa yao apewe mwengine na je kama ni ya Tanganyika kwa Nini isifanyike huko Tanganyika?
    Sijawahi kuona kitu Cha Tanganyika kikifanyika Zanzibar,kinachofanyika Sasa ni kupora haki ya mabondia wa Zanzibar.