Kocha Msaidizi Simba, Juma Mgunda
Habari za michezo

ALICHOSEMA MGUNDA BAADA YA ‘KUITIFUA’ GEITA GOLI 5….KAGERA SUGAR KAZI MNAYO AISEE….

admin December 19, 2022 8:03 am

Licha ya kufanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 kocha Juma Mgunda ameisifu Geita Gold na kusema ni timu nzuri na imewapa ushindani mkubwa.

Mgunda amesema mpira ni mchezo wa makosa ambapo Geita Gold waliyofanya na wao kukayatumia vizuri kupata ushindi mnono.

Mgunda ameongeza kuwa tangu wanatoka Dar es Salaam kwenda Mwanza walikuwa wanajua wanaenda kukutana na timu imara na walijipanga kuwakabili.

“Kupata ushindi mabao matano haimaanishi Geita ni timu mbovu, bali mpira ni mchezo wa makosa wameyafanya tumeyatumia vizuri.

“Jambo jema tumepata alama tatu ugenini tunajipanga kwa mchezo ujao wa ligi dhidi ya Kagera Sugar,” amesema Mgunda.

LICHA YA KUIBUKA NA GOLI 5 …HIZI HAPA REKODI ZA KIBABE ZILIZOWEKWA NA SIMBA JANA.. KAMA ILIKUPITA ,…HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA JANA MGUNDA AKIBEBA TUZO NA ‘MAPESA’ ….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply