Habari za Yanga SC
Habari za michezo

BAADA YA KUUONA MZIKI WA TP MAZEMBE…NABI KAGUNA WEE KISHA AKASEMA HAYA …

admin December 21, 2022 6:59 pm

Licha ya kukiri kuwa wanapaswa kuanza maandalizi mapema ili kufanya vizuri kwenye kundi D la Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Kocha wa Yanga Nasreddine Nabi ameweka wazi mpango wake.

Nabi amesema kuwa akili zao zote kwa sasa wamezielekeza katika kuhakikisha wanafanya vizuri mzunguko wa pili wa Ligi Kuu .

Yanga jumatatu wiki iliyopita walishuhudia droo ya hatua ya makundi ya Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo kikosi chao kimepangwa kundi D pamoja na timu za US Monastir, TP Mazembe na Real Bamako.

Nabi alisema: “Ni kweli tunapaswa kufanya kazi ya ziada ikiwemo kuanza maandalizi ya kikosi chetu mapema kama tunataka kufanya vizuri katika hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika hasa baada ya kuwajua wapinzani wetu.

“Lakini kama timu lazima tuwe na vipaumbele na nikuweke wazi kuwa kwa sasa akili zetu zote ni katika kuhakikisha tunaanza vizuri hesabu za michezo yetu ya mzunguko wa pili kwa kushinda, kama tulivyoshinda mchezo wetu wa kwanza  na wa pili.”

MASIKINI TAMBWE WEEH… YAMKUTA YA KUKUMKUTA NA SINGIDA BIG STARS… TETESI…ILE ISHU YA STRAIKA MGHANA KUTUA SIMBA ‘SHOW’ NZIMA IKO HIVI KUMBE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply