Home Azam FC AZAM FC WAANZA KUWATIA SIMBA SC TUMBO JOTO KWA INONGA…ISHU NZIMA IKO...

AZAM FC WAANZA KUWATIA SIMBA SC TUMBO JOTO KWA INONGA…ISHU NZIMA IKO HIVI..

Habari za Simba SC

SAA chache baada ya kuwavuruga mashabiki na wanachama wa Yanga kwa kumng’oa kibabe kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’, klabu ya Azam FC imedaiwa sasa imeamua kuwageukia Simba SC, ikipiga hesabu ya kumchomoa mmoja ya nyota wa kikosi cha timu hiyo inayoshika nafasi ya pili ya Ligi Kuu Bara.

Azam FC inayoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu, inadaiwa kumalizana na Fei Toto baada ya kiungo huyo kuvunja mkataba kwa kuilipa Yanga Sh112 milioni, zikiwamo Sh12 milioni za mishahara ya miezi mitatu kulingana na vipengele vya mkataba baina yao ili apate nafasi kuondoka.

Lakini, wakati wadau wa soka wakiendelea kujadili dili la Fei na wengine kudhani labda Azam imeshamaliza kasi, matajiri hao wa Bongo wameliamsha tena kwani kwa sasa ikianza mipango ya kumng’oa beki kisiki wa Simba SC, Henock Inonga Baka.

Beki huyo wa kati wa Simba SC kutoka DR Congo ameongeza mkataba utakaomuweka Msimbazi hadi 2025 na Azam FC imefanya mazungumzo na menejimenti yake tayari kumvuta Chamazi kwenda kushirikiana na mabeki wengine wa kati wa timu hiyo.

Habari za kuamini kutoka ndani ya Azam FC zinasema kuwa, mabosi wa timu hiyo wameanza mchakato ili kwenda kuimarisha ukuta wa timu hiyo na mazungumzo kupitia menejimenti ya Mkongoman huyo imefikia pazuri na muda wowote beki huyo atasainishwa mkataba ili aungane na kina Idris Mbombo.

Mmoja ya rafiki wa karibu wa beki huyo, alisema kuwa, pande mbili zipo kwenye mazungumzo mazuri kupitia wakala wa mchezaji, ili atue Chamazi na kulikuwa na ishu ya masilahi ndio hawajamalizana nao.

“Kila kitu kinaonekana kinaenda sawa, tayari mazungumzo yameanza na kilichobaki ni pande mbili kuafikiana kabla ya mabosi wa Azam FC kuwafuata wenzao wa Simba SC ili kukubaliana kwani bado ana mkataba na Azam imeonyesha haitanii kwani ipo tayari kutoa mkwanja wowote,” kilisema chanzo hicho za kuaminika.

Kama Inonga atatua Azam ataungana na Daniel Amoah, Malickou Ndoye pamoja na Abdallah Kheri ‘Sebo’ wanaosimama beki ya kati ya timu hiyo ambayo hadi sasa katika ligi imeruhusu jumla ya mabao 16 katika mechi 17 ikiwa ni wastani wa kila mechi moja imefungwa bao moja.

Inonga alisajiliwa misimu miwili iliyopita na amekuwa mmoja ya mhimili imara wa timu hiyo ambapo kwa misimu yote akishirikiana na Joash Onyango na wakati mwingine ilikuwa Pascal Wawa na Kennedy Juma na kuifanya Simba SC iwe timu ngumu kufungika.

Kwa sasa Simba imeruhusu mabao nane kama iliyofungwa Yanga katika mechi 17 za msimu huu. Msimu uliopita Simba iliruhusu mabao 14 katia mechi 30, huku Azam FC ikifungwa 28 kwa idadi ya mechi kama hizo.

Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin ‘Popat’ alipoulizwa jana juu ya dili hilo, aliiishia kucheka na kusema subiri muda utaongea .

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA AWALETEA JEURI WAKONGWE WA SOKA...AMEIBUKA NA KUCHIMBA MKWARA MZITO