KINARA wa pasi za mwisho ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Simba SC, Clatous Chama ana hatari kila baada ya dakika 104 akiwa uwanjani.
Ni mabao matatu katupia kibindoni akiwa ametoa jumla ya pasi 9 anafuatiwa na Ayoub Lyanga wa Azam FC ambaye ametoa pasi 7 na katupia bao moja.
Simba SC ikiwa imetupia mabao 37 baada ya kucheza mechi 17, nyota huyo kahusika kwenye jumla ya mabao 12 kwa msimu huu.
Kacheza mechi 14 akiwa ameyeyusha dakika 1,252 raia huyo wa Zambia chaguo la kwanza la Kocha Mkuu mzawa Juma Mgunda.
Mchezo ujao kwa Simba SC ni dhidi ya KMC unaotarajiwa kuchezwa Desemba 26, Uwanja wa CCM Kirumba katika mchezo uliopita walitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.
SOMA NA HII KOCHA SIMBA APANGA KUMTIBULIA ZAIDI NABI NDANI YA YANGA...AAPA 'KUMKUSANYA KAMA ZEGE'...