Home Habari za michezo SIMBA SC KUTAMBULISHA KIFAA HIKI KIPYA KESHO UWANJANI…NTIBAZONKIZA KUKINUKISHA..

SIMBA SC KUTAMBULISHA KIFAA HIKI KIPYA KESHO UWANJANI…NTIBAZONKIZA KUKINUKISHA..

Kikosi cha Simba SC Msimu huu wa 2022/23

Wakati kiungo mpya, Saido Ntibazonkiza, anatarajiwa kuanza kuitumikia timu yake ya Simba SC kesho katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons, klabu hiyo huenda ikatangaza mchezaji mpya iliyemsajili kwenye dirisha dogo ambalo limefunguliwa.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, alisema wanatarajia kukamilisha taratibu zote muhimu kesho na mambo yakienda vyema, Ntibazonkiza atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka dimbani kuwakabili Maafande wa Prisons.

Ahmed alisema mchezaji huyo yuko tayari kuongeza nguvu katika kikosi cha Simba SC na wanaamini ujio wake utawasaidia.

“Siku hiyo uwanjani itakuwa ni kama sherehe kwa wanachama na mashabiki wa Simba SC, tunakwenda kuuaga mwaka 2022, kwenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwenda kupongezana Wanasimba, kukosoana na kuulizana kuanzia kwenye timu yetu na hata maisha ya kawaida kama wanadamu, ” alisema Ahmed.

Aliongeza klabu hiyo inaendelea na mchakato wake wa kusajili na huenda pia kesho wakatambulisha mchezaji mpya kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Mwenyekiti wa Bodi (Salim Abdallah) ameniambia analifanyia kazi hilo, likiwezekana atanijulisha kwa hiyo Ijumaa itakuwa ni mechi fulani hivi ya Wanasimba na baada ya hapo wakazi wa Dar na Tanzania Bara hawataiona tena timu kwa sababu itaelekea Zanzibar kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi,” alisema kiongozi huyo.

Aliongeza wanachama na mashabiki wa Simba SC wasikaririshwe majina ya wachezaji wanaodaiwa wanasajiliwa na badala yake wasubiri taarifa rasmi ya klabu.

“Tunaendelea na usajili wa wachezaji wapya, wanachama na mashabiki wa Simba wasiwe na wasiwasi, wanatakiwa kukaa wakisubiri mchezaji yoyote atakayekuja kuisaidia timu na siyo jina la mtu au lazima aje mchezaji fulani,” alisema Ahmed.

Miongoni mwa majina ya wachezji wanaohusishwa na Simba SC ni pamoja na Manzoki anayekipiga China, ambapo taarifa zinasema kuwa dili lake lipo nusu kw nusu kutokana na yeye hivi karibuni kupatwa na majeruhi ambayo yatamuweka nnje ya uwanja mpaka mwezi wa tatu.

Aidha, hivi karibuni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Salim Muhene, Try Again aliweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagram yenye ufanano na mchezaji huyo.

Ukiachana na Manzoki, wengine ni pamoja na Mudathir Yahya aliyekuwa akiichezea Azam FC , Kelvin Nashoni kwa wachezaji wa ndani, huku pia kukiwa na uwezekano wa kuwa na sapraizi ya kumrudisha nyumbani Kiungo wa Al ahly ya Misri, Luis Miquissone.

SOMA NA HII  BAADA YA TANZANIA KUFUZU AFCON MWAKANI....MASTAA WOTE KULAMBA BINGO HILI...