Home Habari za michezo WAMOROCCO WAENDELEA KUITIKISA YANGA SC…WATUMA OFA NZITO KWA AZIZ KI…

WAMOROCCO WAENDELEA KUITIKISA YANGA SC…WATUMA OFA NZITO KWA AZIZ KI…

Habari za Yanga

IMEFAHAMIKA kuwa matajiri wa Klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco wamefunga safari na kuja nchini kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya kumpata kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Mburkinabe, Stephane Aziz Ki.

Hiyo ni mara ya pili kwa Berkane kumfuata kiungo huyo kwa ajili ya mazungumzo ya kuinasa saini yake tangu akiwa katika klabu yake ya zamani ya Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast.

YangaC S iliingia katika vita kali ya kuwania saini ya kiungo huyo dhidi ya Berkane katika usajili mkubwa wa msimu huu kabla ya kushinda na kiungo huyo kuvalia jezi zenye rangi ya njano, kijani na nyeusi.

Mmoja wa mabosi wa Yanga SC, amesema kuwa, wapo wachezaji wengi wanawaowaniwa na baadhi ya klabu za ndani na nje na kati ya hao ni Aziz Ki mwenye kiwango bora hivi sasa.

Bosi huyo alisema kuwa Berkane tayari wametuma ofa kwa uongozi wa Yanga SC kabla ya mabosi wao kutua nchini kwa ajili ya kutua kukamilisha usajili wake kama wakipewa majibu mazuri.

Aliongeza kuwa licha ya kutuma ofa hiyo Berkane, upo ugumu wa Yanga SC kumuachia kiungo huyo kutokana na umuhimu mkubwa alionao katika kuelekea hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Ukiona ofa nyingi zinakuja katika timu kwa baadhi ya wachezaji wako kuhitajikana klabu nyingine kubwa Afrika, basi ujue una kikosi bora.

“Ndivyo kama ilivyokuwa kwetu, tuna wachezaji wengi ambao wamekuwa wakihitajika na klabu nyingine kwa kununua sehemu za mikataba yao waliyoibakisha.

“Hivyo kama uongozi tunajipongeza katika hilo, kama uongozi tumepokea ofa ya Aziz Ki akihitajika na klabu moja kutoka Uarabuni kwa kuleta ofa nono ambayo kama uongozi hatutaweza kuipokea kutokana na michuano mikubwa ambayo tunashiriki ysa kimataifa,” alisema bosi huyo.

Yanga kupitia kwa Rais wake, Injinia Hersi Said alizungumzi hilo kwa kusema kuwa: “Hatutamuachia mchezaji yeyote muhimu kuondoka katika timu, kutokana na malengo tuliyokuwa nayo ya kutengeneza timu bora Afrika.

“Hivyo mchezaji atakayeondoka ni yule ambaye hayupo katika mipango naye, tupo katika hatua nzuri hivi sasa ya kuboresha mikataba ya baadhi ya wachezaji kwa ajili ya kuendelea kubakia hapa.”

SOMA NA HII  JAMANI KUMBE GUARDIOLA NI MTU KAMA WATU WENGINE