Home Habari za michezo DOMAYO ATUA ‘KITASHA’ NAMUNGO FC…STEPHEN SEY NAYE NDANI AISEE…

DOMAYO ATUA ‘KITASHA’ NAMUNGO FC…STEPHEN SEY NAYE NDANI AISEE…

Frank Domayo ajiunga na Namungo FC

Kiungo wa zamani wa Klabu ya Young Africans na Azam FC Frank Domayo ‘Chumvi’ ametambulishwa rasmi na Klabu ya Namungo FC ya mkoani Lindi.

Domayo amejiunga na klabu hiyo akiwa mchezaji huru, baada ya kuachwa na Azam FC mwishoni mwa msimu uliopita 2021/22.

Domayo ametambulishwa rasmi Klabuni hapo kupitia Kurasa na Mitandao ya Kijamii ya timu hiyo, huku taarifa hiyo ikiandikwa:

#WelcomeTosouthernkillers✅ Karibu kwenye Familia ya Namungo Fc Frank Raymond Domayo #Chumvi @domayo #southenkillers

Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa katika timu hiyo katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili, akitanguliwa na Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Stephen Sey.

Sey aliwahi kuitumikia Namungo msimu wa 2020/21 kabla ya kuondoka, baada ya kusajiliwa na Klabu ya Eastern Company SC ya nchini Misri.

SOMA NA HII  HAYA HAPA MAMBO 6 WALIYOPITISHA SIMBA LEO...NAFASI YA MANGUNGU MHHH...KABURU ATOA NENO...