Home Habari za michezo HIVI NDIVYO TFF ‘WANAVYOPIGA PESA’ KWA KILA MCHEZAJI WA KIGENI ANAYESAJILIWA BONGO…..

HIVI NDIVYO TFF ‘WANAVYOPIGA PESA’ KWA KILA MCHEZAJI WA KIGENI ANAYESAJILIWA BONGO…..

Habari za Simba na Yanga

Mpira wa miguu nchini unazidi kukua ambapo wachezaji wa kigeni, makocha na viongozi kwenye nyanja mbalimbali wameongezeka huku Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Idara ya Uhamiaji na Wizara ya Kazi na Ajira zikinufaika kwa mapato kupitia watumishi hao.

Takwimu zinaonyesha ni Sh2.07 bilioni zilizokusanywa na taasisi hizo kutokana na wachezaji wote wa kigeni na mabenchi ya ufundi hadi sasa katika Ligi Kuu Bara, Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake. Kati ya hizo, TFF imenufaika zaidi kwa kuingiza Sh949 milioni (sawa na asilimia 45.6) ya makusanyo yaliyotokana na watu hao.

Idara ya Uhamiaji iliingiza Sh697.8 milioni (sawa na asilimia 33.7), huku Wizara ya Kazi na Ajira ikivuna Sh429.2 milioni (asilimia 20.7).

Katika utoaji wa vibali vya makazi Idara la Uhamiaji kuna tofauti ya malipo kwa watu wanaotoka nchi za SADC ambazo ni Angola, Botswana, Comoro, DR Congo, Eswatini, Lesotho, Madagascar, Malawi, Msumbiji, Mauritius, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe, na nchi za Ulaya hulipa Sh4.7 milioni kila mtu kwa mwaka.

Wakati nchi za Afrika Mashariki ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Sudan Kusini, DR Congo na Burundi malipo yao ni Sh2.3 milioni kila mtu kupata kibali cha makazi, huku Wizara ya Kazi na Ajira wanaotoa vibali vya kazi mtu mmoja hulipiwa Sh2.3 milioni. Msemaji wa Idara ya uhamiaji nchini, Paul Mselle ameliambia Mwanaspoti kuwa wanatoa kibali cha makazi baada ya mhusika kupata kibali cha kazi kwa kutegemea aina ya mkataba wake na nchi anayotoka.

TFF huvuna Sh4 milioni kwa kila mchezaji na Sh6.9 milioni kwa kocha kwa msimu na hii ni kwa mujibu wa kanuni ambao jumla wapo 24 kati ya wafanyakazi wote 188. Lakini Ofisa Habari za Shirikisho la Soka la Tanzania, Clifford Ndimbo alipoulizwa kuhusiana na utaratibu huo alisema mgeni yoyote lazima alipie ada zilizowekwa kwa mujibu wa kanuni na kiasi hicho ni kwa mchezaji au mfanyakazi yoyote raia wa kigeni kabla ya kuanza kazi.

LIGI KUU BARA (123)

SIMBA – 15

Clatous Chama (Zambia), Joash Onyango (Kenya), Henock Inonga (DR Congo), Sadio Kanoute (Mali), Pape Sakho (Senegal), Peter Banda (Malawi), Moses Phiri (Zambia), Augustine Okrah (Ghana), Victor Akpan (Nigeria), Nelson Okwa (Nigeria), Mohamed Ouattara (Ivory Coast) na Dejan Georgijevic (Serbia) na jumla ya wachezaji ni 11.

Katika benchi la ufundi Simba kuna Kelvin Mandla (kocha wa viungo -Afrika Kusini), Chlouha Zakaria (kocha wa makipa – Morocco) na Culvin Mavunga (msoma takwimu – Zimbabwe).

YANGA – 16

Wachezaji wa Yanga wageni ni Djigui Diarra (Mali), Djuma Shaban (DR Congo), Yanick Bangala (DR Congo), Khalid Aucho (Uganda), Fiston Mayele (DR Congo), Herritier Makambo (DR Congo), Azizi Ki (Ivory Coast), Bernard Morrison (Ghana), Tuisila Kisinda (DR Congo), Jesus Moloko (DR Congo), Joyce Lomalisa (DR Congo) na Gael Bigirimana (Burundi)

Katika benchi la ufundi kuna Nasreddine Nabi (kocha mkuu – Tunisia), Cedric Kaze (kocha msaidizi – Burundi), Helmy Gueldich (viungo -Tunisia) na mtendaji mkuu, Andre Mtine (Zambia).

Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Saad Kawemba alifafanua kwamba; “Ni gharama kubwa sana ambayo kama klabu tunalipa, ni kama Sh10milioni kwa mchezaji mmoja ili utaratibu wake ukamilike na vyote hivyo vinalipwa kabla ya yote. Hapo bado ada ya uhamisho na masilahi ya mchezaji au mgeni husika.”

AZAM – 16

Wachezaji wa Azam FC ni Ali Ahamada (Comoro/Ufaransa), Malickou Ndoye (Senegal), Bruce Kangwa (Zimbabwe), Daniel Amoah (Ghana), Isah Ndala (Nigeria), James Akaminko (Ghana), Kenneth Muguna (Kenya), Rodgers Kola (Zambia), Idris Mbombo (DR Congo), Prince Dube (Zimbabwe), Kipre Junior (Ivory Coast) na Tape Edino (Ivory Coast).

Kwenye benchi la ufundi kuna Denis Lavagne (Ufaransa) aliachwa, Abdihamid Moallin (alibadilishiwa majukumu – Marekani), Dani Cadena (makipa – Hispania) na Mikel Guillen (viungo – Hispania).

SINGIDA BIG STARS – 15

Ndani ya Singida Big Stars wachezaji ni Pascal Wawa (Ivory Coast), Carno Biemes (DR Congo), Meddie Kagere (Rwanda), Amissi Tambwe (Burundi), Nicolus Gyan (Ghana), Shafiq Batambuze (Uganda), Bruno Gomes (Brazil), Rodrigo Carvalho (Brazil), Dario Frederico (Brazil), Peterson Cruz (Brazil) aliyeondoka karibuni, Miguel Escobar (Argentina) na Joel Madondo (Uganda).

Katika benchi la ufundi kuna Hans Pluijm (kocha mkuu – Uholanzi), Mathias Lule (kocha msaidizi – Uganda) na Ramadhan Nswanzurino (mkurugenzi wa ufundi – Burundi).

POLISI TANZANIA – 5

Katika kikosi hiki wachezaji ni Ambrose Awio (Uganda), Sosthenes Khakali Idah (Kenya), Blanchard Ngabonziza (Burundi) na Shaban Mabano (Burundi). Kwenye benchi la ufundi kuna

Mwinyi Zahera (kocha mkuu – DR Congo).

NAMUNGO FC – 10

Wachezaji wa Namungo ni Jonathan Nahimana (Burundi), Christopher Okoje (Kenya), Emmanuel Asante (Ghana), Alidor Kayembe (DR Congo), Hugues Ininahazwe (Burundi), Baba-Seido Blandja (Togo), Blessing Godwin (Nigeria), Smith Dohemeto (Benin) na Sedjro Counou (Benin). Katika benchi la ufundi yupo Hanour Janza (kocha mkuu – Zambia) anayedaiwa kuondoka.

MTIBWA SUGAR – 6

Wachezaji ni Farouk Shikhalo (Kenya), lakini ameondoka, Deo Kanda (DR Congo), Pascal Kitenge (DR Congo), James Kotei (Ghana), Matore Jean Pipi (Burundi) na Mayanja Brian (Uganda).

MBEYA CITY – 3

Wachezaji ni Ssemujju Joseph na Hassan Muhamud (Waganda) na benchi la ufundi liko chini ya Abdallah Mukuru (kocha mkuu – Uganda).

KMC – 5

Wachezaji ni Emmanuel Mvuyekure (Burundi), Nzigamasabo Styve (Burundi), Bigirimana Blaise (Burundi) na Nouridine Balora (Burkina Faso), huku benchi la ufundi yupo Thiery Hitimana (kocha mkuu – Burundi).

IHEFU FC – 4

Wachezaji ni Never Tigere (Zimbabwe), Nico Wadada (Uganda), James Ssetuba (Uganda) na Papy Tshishimbi (DR Congo) na Obrey Chirwa (Zambia).

GEITA GOLD – 5

Wachezaji ni Said Ntibazonkiza (Burundi), Eric Yema Lyomi (DR Congo), Arakaza Mac Arthur (Burundi), Shawn Oduro (Ghana) na Shinobu Sakai (Japan).

DODOMA JIJI – 4

Wachezaji ni Christian Zigah (Ghana), Opare Collins (Ghana) na Randy Bangala (DR Congo) huku benchi la ufundi yupo Melis Medo (kocha mkuu – Marekani).

COASTAL UNION – 9

Wachezaji ni Joseph Zziwa (Uganda), Emiry Nimubona (Burundi), Gerard Moubarack (Cameroon), Djibril Naim (Benin), Pembele Muanisa Rigue (DR Congo), Betrand Kunfor Ngafei (Cameroon), Mahamud Mroivili (Comoro) na Cedrick Mavugo (Burundi) na benchi la ufundi yupo Yusuph Chipo (kocha mkuu – Kenya).

KAGERA SUGAR – 5

Wachezaji ni Hamisi Kiiza, Deus Bukenya, Jackson Kibirige (wote Uganda), Stephen Duah (Ghana) na Appoliniare Ngueko (Cameroon).

TANZANIA PRISONS -2

Mchezaji ni Joshua Otieno (Kenya) na benchi la ufundi kuna Patrick Odhiambo (kocha mkuu-Kenya).

RUVU SHOOTING

Timu haina mchezaji wa kigeni.

LIGI YA CHAMPIONSHIP (21)

AFRICAN SPORT – 1

Mchezaji ni Kilumba Nkomba (DR Congo)

BIASHARA UNITED – 1

Mchezaji ni Mathew Odongo (Uganda).

FOUNTAIN GATE FC -7

Wachezaji ni Stephen Orare, Dennis Wanyoike, Maroa Nchagwa, Kabaji Wyciffe, Kelvin Mwavali, Kelvin Sagida (wote Kenya) na Owen Chaima (Malawi)

KITAYOSCE FC – 10

Wachezaji ni Jordan Sungu, Daniel Chal, Ngeleka Katembua, Guylain Kisombe, Fabrice Ngoy, Pele Ngulakwey (wote Congo), Collins Gyamfi, Asante Kwasi na Emmanuel Lamptey (wote Ghana), John Nakibinge (Uganda).

MBEYA KWANZA -1

Mchezaji ni Raphael Aloba (Nigeria).

PAMBA FC – 1

Mchezaji ni Kabamba Erick (Zambia). Timu ambazo hazina wachezaji wa kigeni Championship ni Green Warriors, Gwambina FC, JKT Tanzania, Transit Camp, Copco, KenGold, Mashujaa, Mbuni, Ndanda na Pan African.

FIRST LEAGUE (Jumla 5)

AFRICAN LYON – 2

Wachezaji ni Joshua Kigoz (Uganda) na Fidel Houinsa (Benin).

DAR CITY – 3

Wachezaji ni Serge Abdallah Biaya, Patrick Ndibu Mayumba, Lukis Djese Lukamba (wote DR Congo). Kwenye First League timu ambazo hazijasajili wachezaji wa kigeni ni Kasulu, Kurugenzi, Lipuli, Majimaji, Mbao, Mwadui, Njombe Mji, Rhino Rangers, Stand United, TMA Stars, TRA Kilimanjaro na Tunduru Korosho.

LIGI KUU YA WANAWAKE (Jumla 38)

SIMBA QUEENS – 11

Wachezaji ni Pambani Kuzoya, S’arrive Badiambila, Daniela Ngoyi (wote DR Congo), Barakat Olaiya (Nigeria), Joelle Bukuru, Asha Djafari (wote Burundi), Vivian Corazone, Topister Situma, Philomena Abakah (Ghana) na Carolyne Rufa (Kenya) huku benchi la ufundi yupo Charles Lukula (kocha mkuu – Uganda).

YANGA PRINCESS – 12

Wachezaji ni Tessy Biahwo, Mary Saiki, Prescious Onyinyechi, Blessing Nkor, Wogu Success (wote Nigeria), Salifu Safiatu (Ghana), Wingate Kaari, Pauline Kathuruh, Foscah Kanenge (wote Kenya), Aniella Uwimana (Burundi), Marry Mushiya (DR Congo) na Nadege Atanhloueto.

ALLIANCE GIRLS – 4

Wachezaji ni Akinyi Otieno, Anita Adongo, Florida Omusanga (wote Kenya) na Adelaide Nimfasha (Burundi).

FOUNTAIN GATE PRINCESS – 7

Niyonkuru Sandrine (Burundi), Peris Oside, Myline Awuor, Inviolata Mukoshi, Amakobe Esther na Chebeti Monicah (wote Kenya), huku benchi la ufundi ni Alex Alumirah (kocha mkuu, Kenya).

RUVUMA QUEENS – 3

Wachezaji ni Dorothy Mukatasha (Zambia), Munezero Umurundi na Bukuru Rachele (wote Burundi).

THE TIGER QUEENS -1

Mchezaji ni Charlotte Irankunda (Burundi). Kwenye ligi hiyo timu za Amani Queens, Ciassia Queens, Baobab Queens na JKT Queens hazikusajili wachezaji wa kigeni.

SOMA NA HII  SIMBA YAJIBU KILIO CHA MASHABIKI....KAZI KUANZA RASMI KESHO...CHAMA MAPEMA TU....