Home Habari za michezo KIBU DENIS AFUNGUKA ISHU YAKE YA KWENDA ULAYA…ATAJA WALIOMSAIDIA…

KIBU DENIS AFUNGUKA ISHU YAKE YA KWENDA ULAYA…ATAJA WALIOMSAIDIA…

Habari za Simba

Baada ya kufunga bao lake la kwanza kwenye Ligi Kuu msimu huu, nyota wa Simba Kibu Denis amekiri kupitia kipindi kigumu, lakini sasa kila kitu kimekuwa sawa na yupo tayari kwa mapambano, huku akifungukia ishu ya kupumzika Ufaransa.

Kibu aliyekuwa kinara wa mabao Simba msimu uliopita akitikisa nyavu mara nane, msimu huu haujaanza vizuri kwake na kuonekana kushuka kiwango lakini baada ya juzi kufunga bao moja Wanamsimbazi wakishinda 5-0 amefunguka hali aliyokuwa akipitia.

Nyota huyo wa zamani wa Kumuyange, Geita Gold na Mbeya City alisema alikuwa akipitia kipindi kigumu lakini anawashukuru viongozi wa Simba, wachezaji na benchi la ufundi kwa kuwa naye pamoja na kumsaidia kurudi kwenye ubora.

“Nilipitia kipindi kigumu ambacho kila mchezaji huwa anapitia lakini tofauti ni ukubwa, nawashukuru waachezaji, makocha, viongozi na mashabiki wote wa Simba kwa kunivumilia na kuwa pamoja katika kipindi hicho,” alisema Kibu na kuongeza;

“Nimefurahi kufunga leo (juzi), nadhani huu ndio mwanzo mpya kwangu na nitaendelea kufanya vizuri kila nikipewa nafasi.”

Simba ili kuhakikisha Kibu anarejea kwenye ubora wake alioanza kuunyesha juzi, ilimpa mapumziko ya siku tano na aliyatumia kwenda Ufaransa kupumzika na baadhi ya watu wake wa karibu na aliporudi Bongo alikuwa na muda maalumu wa kuongea na Kocha Juma Mgunda na wasaidizi wake ili kuhakikisha anakuwa sawa kisaikolojia.

Hata kabla ya mechi hiyo, inaelezwa kibu alikaa zaidi ya nusu saa na benchi la ufundi akipewa maelekezo na kumjenga ili kuondoa presha na kucheza kwenye ubora.

“Nilipewa mapumziko nikaenda Ufaransa, baada ya kurudi ndiyo nimeanza vizuri, nafikiri huu ni mwanzo sasa nitaendelea kufanya bora sana,” alisema Kibu.

GEITA, IHEFU ZAMUWANIA

Wakati Kibu akiendelea kurejea kwenye makali yake, klabu za Geita Gold na Ihefu zimetuma ofa Simba kutaka saini ya mshambuliaji huyo kwa mkopo kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Mwanaspoti limethibitisha Geita wapo kwenye kusuka upya kikosi chao na pendekezo la kwanza eneo la ushambuliaji ni Kibu ambaye wanaamini atarithi mikoba ya George Mpole aliyetimkia FC Lupopo ya DR Congo.

Bado Simba na Kibu hawajajibu ombi hilo la Geita aliyoichezea kipindi ipo (Daraja la kwanza) kwa sasa Chamiponship.

Wakati huo huo, taarifa kutoka Mbeya zinaeleza Ihefu nayo ipo kwenye hatua za mwisho za kutuma ofa Simba kumuomba Kibu kwa mkopo.

Wakati timu hizo mbili zikiwania saini ya Kibu, Simba ndiyo itaamua imtoe kwa mkopo au imuache kikosini kwani bado ana mkataba wa miaka miwili na mabosi hao wa Msimbazi.

SOMA NA HII  SIMBA YAPANIA KUFANYA VIZURI KIMATAIFA