Home Habari za michezo KISA MESSI KUITWA ‘G.O.A.T’…EDO KUMWEMBE AIBUKA NA KUWEKA REKODI SAWA…AMTAJA RONALDO…

KISA MESSI KUITWA ‘G.O.A.T’…EDO KUMWEMBE AIBUKA NA KUWEKA REKODI SAWA…AMTAJA RONALDO…

Mchambuzi maarufu wa michezo nchini, Edo Kumwembe amepinga suala la nahodha wa Argentina, Lionel Messi kuitwa GOAT kisa kutwaa Kombe la Dunia.

Huwa nina mawazo tofauti kuhusu suala la GOAT. Jana nilikuwa nawasoma wachambuzi wa Ulaya. Ni kama vile wamehitimisha mjadala wa GOAT baada ya Messi kutwaa World Cup.

Hii issue ya kwamba GOAT huwa anapatikana wakati wa World Cup huwa siihafiki. Ililetwa na wazee wa zamani kwa ajili ya kuhakikisha Pele na Maradona hawagusiki.

Zamani pia World Cup kilikuwa kitu kikubwa zaidi kwa sababu wachezaji asilimia 99 walikuwa wanacheza home. World Cup ndio ilikuwa sehemu pekee ya kuonyeshana umwamba.

Siku hizi maisha yamebadilika na wachezaji wengi wanacheza ugenini na kuonyeshana umwamba. Hata kama Messi asingechukua World Cup jana hauwezi kuniambia eti sio GOAT.

Hauwezi kuniambia Cristiano sio GOAT kwa sababu hajawahi kutwaa World Cup. Lakini World Cup ina mazingira mengi ya kushinda. Kikosi imara plus bahati.

Thomas Lemar kachukua World Cup lakini Ronaldo hajachukua. Kolo jana angemfunga Martinez France ingetwaa World Cup ina maana Messi asingekuwa GOAT? Binafsi hawa akina GOAT wanapatikana kwa namna wanavyocheza kila wikiendi na sio World Cup tu.

Kama naamini Messi ni bora kuliko Ronaldo sidhani kwa sababu ametwaa World Cup jana. Namkubali Messi lakini Ronaldo pia ni GOAT.

Haya mambo ya kuambiana GOAT anapatikana katika World Cup niliyapinga kabla Messi hajatwaa World Cup jana, na nitaendelea kupinga. World Cup ina mechi 7 ndani ya miaka minne wakati Ligi na michuano mingine ina mechi 49 kwa msimu. Sijui nimeeleweka? – amesema Edo Kumwembe.

SOMA NA HII  JAMA JAMA LITAKUFA JITU AISEEE....KWA SIMBA HII IJAYO WEKA MBALI NA WATOTO...MO DEWJI HATAKI MASIKHARA KABISA...