Home Uncategorized KESHO NI DODOMA JIJI V RUVU SHOOTING UWANJANI

KESHO NI DODOMA JIJI V RUVU SHOOTING UWANJANI

 


KESHO Oktoba 2 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea kuchanja mbuga ikiwa ni raundi ya tano sasa baada ya raundi ya nne kukamilika na kushuhudia jumla ya mabao 13 yakifungwa kwenye mechi tisa zilizochezwa.


Ruvu Shooting ambayo mchezo wake uliopita ilikuwa Uwanja wa Uhuru na ililazimisha sare ya bila kufungana na Biashara United inashuka Uwanja wa Jamhuri Dodoma kumenyana na Dodoma Jiji.


Dodoma Jiji wao wametoka kupokea kichapo cha mabao 3-0 na Polisi Tanzania ambapo shujaa aliyewatungua mabao mawili Uwanja wa Ushirika Moshi alikuwa ni Marcel Kaheza nyota wa Polisi Tanzania.

Dodoma Jiji wakiwa Uwanja wa Jamhuri wamecheza mchezo mmoja ilikuwa ni dhidi ya Mwadui FC, Septemba 6 na ilishinda bao 1-0.

SOMA NA HII  MITAMBO HII NANE YA KAZI YAINGIA ANGA ZA YANGA