Home Habari za michezo MASTAA YANGA WAANZA KUKINUKISHA….MORRISON NAYE NDANI…

MASTAA YANGA WAANZA KUKINUKISHA….MORRISON NAYE NDANI…

Habari za Yanga

Kikosi cha Timu ya Yanga jana Alhamisi, Desemba 1, 2022 kimeanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons kambini Avic Town, Kigamboni dar es Salaam.

Awali, wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja baada ya Kutoka jijini Mbeya Kwenye mchezo dhidi ya Ihefu sc ambao walipoteza kwa kufungwa mabao 2 kwa 1.

Aidha, baadhi ya wachezaji tegemeo waliokuwa majeruhi katika kikosi hicho wamerejea mazoezini.

Wachezaji wamerudi mazoezini na taarifa njema ni kurudi kikosini wachezaji Kama.

Feisal Salum ‘Fei Toto’ ameanza mazoezi na wenzake jana kambini baada ya kumaliza matibabu kutoka kwenye jopo la madaktari wa Yanga.

Benard Morrison amerudi mazoezi baada ya kupona majeraha yake ya kifundo cha mguu (enka).

Djuma Shabani ‘Soda ya Bemba’ amerejea kikosini jana na kufanya mazoezi na wenzake kambini Avic Town. Djuma Shabani alikuwa anasumbuliwa na tatizo la nyama za paja kwa sasa yupo fiti kurejea kikosini.

Heritier Makambo anatarajiwa kuanza mazoezi hapo leo asubuhi. Makambo alikuwa na jeraha kwenye kidole chake cha mguu wa kushoto akiwa nchini Tunisia wakati wa maandalizi ya mwisho Kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Club African.

Bakari Nondo Mwamnyeto amerejea kikosini na ameanza mazoezi jana kambini sambamba na wezni. Mwamnyeto alipata majeraha wakati wa mazoezi Sokoine Mbeya wakijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ihefu sc.

Crispin Ngushi yupo fiti ana amejiunga na wenzie mazoezi jana. Kwa sasa Ngushi amepona jeraha lake la goti na Yupo kamili kuwatumikia Wananchi.

Kiungo fundi, Farid Mussa Malick ataungana na Makambo hapo leo kwenye mazoezi kambini Avic Town.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI