Home Habari za michezo KIWANGO CHA BOCCO CHAWAVURUGA MABOSI MSIMBAZI…WASHINDWA KUAFIKIANA ISHU YA KUACHANA NAYE…

KIWANGO CHA BOCCO CHAWAVURUGA MABOSI MSIMBAZI…WASHINDWA KUAFIKIANA ISHU YA KUACHANA NAYE…

Habari za Simba SC

Nahodha John Raphael Bocco anatajwa kuwavuruga viongozi na mashabiki wa Simba kufuatia kufunga magoli manne katika mechi tatu za Simba za hivi karibuni ambapo alifunga magoli 3 dhidi ya Ruvu Shooting na goli 1 dhidi ya Polisi Tanzania kule Moshi.

Kabla ya mechi hizo John Bocco aliyeipa mafanikio makubwa timu ya Simba akitokea Azam FC hakufunga goli lolote toka mwanzo wa msimu hali iliyopelekea jina lake kutajwa katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa kuachwa na Simba SC katika dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kufunguliwa Desemba 15 mwaka huu.

Bila shaka ufungaji wake wa magoli unawafanya viongozi na benchi la ufundi la Simba kukuna vichwa vyao na kulitazama jina la mkongwe huyo mara mbili mbili kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho.

SOMA NA HII  EDO KUMWEMBE: TATIZO SIMBA SIO WAVUMILIVU UGENINI...HATA WANGESHINDA 2-0 BADO WASIWASI UNGEKUWEPO...